26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge adai wananchi Lindi wafupi sababu ya kubeba mizigo kichwani

Arodia Peter, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, Riziki Lulida (CUF), amesema wananchi wa mkoa huo wanakuwa wafupi kwasababu ya kubeba mizigo kichwani kwa kukosa usafiri kupitia barabara.

Lulida ameyasema hayo bungeni leo Mei 10, ambapo amesema kuwa Mkoa huo umekuwa ukitengwa kila mwaka kwa kunyimwa miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwamo ya barabara.

Lulida ametolea mfano wa barabara za jimbo la Liwale kwamba hazikuwahi kujengwa kwa kiwango cha lami tangu serikali ya awamu ya kwanza.

“Mheshimiwa Naibu Spika kuna ubaguzi unafanywa na mawaziri katika kugawa miradi hapa nchini, huko Lindi  Liwale tumekuwa kama Guantanamo,  ninashauri Bunge tutengue kauli ya kuapa kwa kutumia biblia au quran, tutumie katiba badala ya hiyo misahafu kwa sababu hivyo vitabu havitaki uongo.

“Niwaambie huko Lindi mnazuia kangomba ya korosho wakati hamjengi barabara,  wale wafanyabiashara wanaamua kupeleka magari yao hata kwa shida lakini mnawazuia kununua korosho, je mnataka watu wafanyeje, leo hii watu wa Lindi wamekuwa wafu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles