23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

MBUNGE ADAI KUPAPASWA

Na Fredy Azzah-Dodoma


MBUNGE wa Kavuu, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), amedai kuwa walinzi wanaowakagua wakati wakiingia kwenye viwanja vya Bunge, wanawapapasa sehemu mbalimbali za miili yao.

Mbunge huyo alisema hayo jana wakati akiomba mwongozo wa kiti, jambo lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kupiga marufuku ukaguzi wa aina hiyo.

Alisema wanapopita kwenye mashine za ukaguzi hutakiwa kuvua mikanda, viatu, saa na vitu vingine na kwamba kibaya zaidi kwake ni suala la kupapaswa.

“Tunavua nguo, watu wanainua mashati kuvua mikanda na tunaona vitovu vya wanaume halafu miili inasisimka tukidhani wanataka kufanya maandalizi, mwili wa mwanadamu una vivutio vingi.

“Leo nimepita mashine moja vizuri na nilipofika ya pili ikalia. Nikaambiwa nikaguliwe sasa kibaya nakwenda kukaguliwa ananishikashika maeneo mbalimbali, hapa tuna mwezi mmoja huku si kutiana hanjamu?,” alihoji.

Dk. Kikwembe alimtaka Spika kutoa agizo kukomesha jambo hilo, akisema halikubaliki na lina wadhalilisha wabunge kila wakati.

Naye Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), aliomba mwongozo akilalamikia wabunge kulazimishwa kuvaa vitambulisho wawapo eneo la Bunge.

Akijibu miongozo hiyo, Spika wa Bunge, Ndugai aliagiza ukaguzi kwa kuwashikashika wabunge mwilini uachwe mara moja kwa kuwa unawadhalilisha.

Ndugai aliagiza utaratibu ufanyike kwa kuangalia namna bora ya kuwakagua wabunge na kwamba kinachofanyika ni ukaguzi wa kizamani uliopitwa na wakati.

“Kwa watumishi sawa, lakini wabunge wangu wanapoingia kuna maeneo kunakuwa na picha zao na wanaonekana kabisa sasa suala la kushikana tena mbona halifai.

“Hivi ukaguzi gani hata unamshika mtu katika maeneo ya mwili wake bila kutumia kifaa, jambo hilo liachwe,” alisema Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles