Arodia Peter, Dodoma
Mbunge wa Tandahimba, Katani Katani amesema biashara ya Kangomba si dhambi kama ambavyo imetafsiriwa na serikali.
Akichangia mjadala wa hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara bungeni leo, Mei 15, Katani amesema kuwa kupitia mauziano kwa mtindo wa kangomba, wakulima wamekuwa wakinufaika kwa kukopeshwa nyenzo za kilimo.
“Mheshimiwa Naibu Spika, biashara ya Kangomba imeruhusiwa hata kwenye vitabu na hadithi za Mtume Muhamad, kangomba si biashara haramu, ni halali kwani humsaidia kupata nyenzo za kilimo kwa makubaliano kwamba akiuza atamfidia yule aliyempa nyenzo.” amesema Katani.