29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MBUNGE ACHANGIA UJENZI WA VYOO VYA SHULE

                                                                 |Mohamed Hamad, ManyaraMbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Ester Mahawe (CCM), ameahidi kutoa mabati na mifuko ya saruji itakayohitajika kujenga vyoo vya Shule ya Msingi Sinai.

Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, shule hiyo ina matundu mawili ya vyoo huku ikiwa na wanafunzi 800.

Mbunge huyo amesema yeye ni mwakilishi wa  wananchi hivyo haoni sababu ya kuacha adha adha hiyo endelea kwa wanafunzi hao na kudai ataondoa tatizo hilo.

“Naahidi kutoa mabati hayo na saruji kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule hii nikiwa kama mzazi na mwakilishi wa wananchi,” amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wamesema kwa sasa wanapata taabu ya kupata huduma hiyo.

“Tuna tatizo kubwa, wakati mwingine tunachelewa kuingia darasani kwa sababu ya kusubiriana kuingia chooni,” amesema mmoja wa wanafunzi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles