24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mbowe, wengine 13 wakamatwa na Polisi

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limewakamata watu 14 wakiwamo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokaidi amri ya Jeshi hilo ya kusitisha maandamano leo Septemba 23, 2024.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema viongozi wa CHADEMA walikamatwa ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na Godbless Lema.

Aidha, amewataka Watanzania wapuuze taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kuwa watu hao wametekwa, bali wamekamatwa na wanaendelea na mahojiano ili taratibu za kisheria ziendelee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles