22.7 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mbowe, Matiko huru kwa dhamana

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,  imetengua uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuwafutia dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, ambapo wameruhusiwa kuwa nje kwa dhamana.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo leo Alhamisi Machi 7, Jaji wa mahakama hiyo aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Jaji Sam Rumanyika, amesema Mahakama imeikubali rufani hiyo kama ilivyo kwa hiyo warufani wanatakiwa wawe nje kwa dhamana kwani uamuzi wa kuwafutia dhamana ulifanyika mapema mno (pre mature).

“Aidha, sharti la kuripoti polisi kila alhamisi limefutwa badala yake watariporti mahakamani mara moja kwa mwezi si polisi tena kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kisutu mara ya kwanza,” amesema.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwafutiwa Mbowe na Matiko dhamana kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana hiyo ambapo walikata rufaa Mahakama Kuu Desemba mwaka jana na uamuzi kutolewa leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles