22.7 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mbowe: Mashitaka yetu ni ya kisiasa

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mashtaka yanayowakabili ni ya kisiasa, yanayoficha waliokosa na kuwahukumu waliokosewa.

Mbowe aliyeanza kujitetea Novemba 4 na 5, mwaka huu, alidai hayo jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Mbowe ameeleza hayo baada ya kuulizwa na wakili Kibatala nini kauli yake kuhusu mashtaka yanayowakabili.

Wakili wake, Peter Kibatala, alimuuliza katika hati ya mashtaka liliibuka suala la kutompenda Rais John Magufuli, na kumuuliza kama anampenda au anamchukia kiongozi mkuu huyo wa nchi.

“Mawazo yangu nikiwa Kiongozi Mkuu wa Chama cha upinzani na Rais Magufuli kiongozi wa Chama Tawala, ameshindwa kusimamia demokrasia katika taifa,”alidai Mbowe lakini hakuendelea kufafanua hilo baada ya Hakimu Simba kuzuia kufanya hivyo.

Katika kesi hiyo Mbowe na wenzake wanane wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kuhamasisha hisia za chuki.

Pia, wanadaiwa kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi  makosa yanayodaiwa kutendeka kati ya Februari 1 na 16, 2018 jijini Dar es Salaam.

Jana Mbowe alimaliza utetezi wake huku akidai katika mchakato wa uchaguzi wa marudio Jimbo la Kinondoni, Chadema waliandika barua mbalimbali Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo kuhusu mawakala wa kusimamia uchaguzi.

Mbowe alidai barua hizo zilikuwa zinatoka Chadema kwenda tume na tume kwenda Chadema kwa nyakati tofauti kuanzia Februari 9, 14 na 15 mwaka 2018.

Mshtakiwa huyo aliomba kutoa barua hizo kwa utambuzi mahakamani na wahusika wakifika kutoa ushahidi watazitoa kama kielelezo na mahakama ilikubali kuzipokea.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali, Salim Msemo, Mbowe alidai kuwepo kwa ngome yao Magomeni ni mila ya chama si Serikali.

Alidai ngome ni nembo yao Chadema hakuna mahali ambapo imeandikwa na kwamba Mkurugenzi wa Uchaguzi anaifahamu ofisi hiyo lakini hakuna barua iliyopelekwa kwake kumfahamisha.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali Jacqline Nyantori, Mbowe alidai matukio aliyoyasema likiwamo kupigwa risasi kwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kutoroshwa kwa Msaidizi wake Ben Saanan, kuuawa kwa Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi na polisi na makada wa CCM, wakati yanatokea hakuwepo.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali, Joseph Pande Mbowe alidai alihutubia katika kampeni ya mwisho ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni kwa kutumia nahau yaani kuiwasilisha ujumbe kwa njia ya mifano.

Mbali na Mbowe,  washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni naibu makatibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara).

Wengine ni mbunge wa mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Halima Mdee (Kawe); Este Bulaya (Bunda), Esther Matiko (Tarime Mjini); John Heche (Tarime Vijijini); Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na  katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles