24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE AVUNJA UONGOZI RUNGWE

Na IBRAHIM YASSIN-RUNGWE


 

freeman-mboweMWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja uongozi wa Jimbo la Rungwe, wilayani Rungwe, ili kukinusuru chama kupasuka kutokana na makundi yanayotishia kukigawa.

Mbowe alichukua uamuzi huo jana wakati wa kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya na majimbo wilayani humo na baadaye kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi hadi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama mwakani.

Kabla ya uamuzi huo, Mbowe alisikiliza hoja za kila mjumbe na kugundua kutoelewana miongoni mwa viongozi, kulikotokana na kura za maoni ngazi ya kata na majimbo kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Uongozi huo wa muda utaongozwa na  Mwenyekiti Sefu Suleiman, Katibu Mwaijumba Mwaijumba na wajumbe 20 ambao watafanya kazi wilaya mzima hadi uchaguzi mpya utakapofanyika. 

“Nimepata taarifa za kuwapo kwa viongozi uchwara wilayani Rungwe ambao wanatishia afya na uhali wa chama chetu, hivyo ili kuleta afya katika chama, nimewaweka pembeni, tunataka kujenga uwajibikaji na si ubabaishaji,” alisema Mbowe.

Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa Chadema Kata ya Ushirika, Baraka Mwampamba, alisema anaunga mkono uamuzi huo wa Mbowe kwani mpasuko huo ulitishia kukivunja chama.

“Wamechokoza chui kwenye kichaka chake, alichokifanywa mwenyekiti ni sahihi kwa masilahi ya chama,” alisema Mwampamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles