28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbowe atangaza mikutano ya hadhara, polisi yaonya

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuanzia Aprili 4, mwaka huu  kitaanza rasmi mikutano ya hadhara nchi nzima.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alisema ajenda kubwa katika mikutano hiyo itakuwa ni kudai tume huru ya uchaguzi na mazingira ya uchaguzi mkuu unoatarajiwa kufanyika Oktoba.

Aliwataka viongozi wote katika ngazi mbalimbali za chama hicho kuanza kujiandaa kufanya mikutano hiyo huku akitamba kuwa wako tayari kwa lolote.

“Hatutasubiri kibali cha mtu yeyote, tarehe nne mwezi wa nne tutaanza mikutano nchi nzima, na kwa kauli hii nawatangazia wabunge, viongozi wote wa kanda, mikoa, wilaya, vijiji, vitongoji hadi mitaa kufanya mikutano ya hadhara kwa utaratibu uliopo kisheria. 

“Tutadai vitu viwili, tume huru na maandalizi ya uchaguzi mkuu, Mbowe, tuna imani mamlaka husika zitatumia busara kuwezesha chama hicho kifanye mikutano hiyo,” alisema Mbowe. 

Hata hivyo Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, alikitahadharisha Chadema kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na kuonya kuwa yeyote atakayejaribu kuvunja sheria atashughulikiwa.  

“Sisi jeshi la polisi tunasimamia sheria, yeyote yule awe nani hatuangalii cheo au rangi ya mtu, kama lengo lake ni kuvunja amani yetu au kuleta vurugu katika nchi atashughulikiwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,” alisema Misime.

Katika hatua nyingine, Mbowe alilaani kitendo cha kushambuliwa kwa baadhi ya wafuasi wa chama hicho wakiwemo wabunge na kuviomba vyombo vya dola kuacha kutumia nguvu za ziada.

“Siku ya tukio mimi na Heche tuliondoka kwenda kufanya kazi shamba la mikorosho, baadaye Heche aliletewa ujumbe anatakiwa jengo la utawala kukamilisha taratibu za kutoka.

“Kwenye saa 7 – 8 (mchana) tukiwa na wafungwa wengine tukasikia filimbi inapigwa gerezani, ikapigwa filimbi ya pili kisha zikaanza kupigwa filimbi mbalimbali. Hadi kipindi kile sikujua kwamba wanaopigiwa fiimbi ni viongozi wamama wa chama chetu…baadaye nikapata taarifa wameshambuliwa.

“Viongozi walikuja kunipokea wakijua nimemaliza taratibu za kulipa faini, kutegemea nitatoka mwenyewe bila kupokelewa haiwezekani, mimi ni mwenyekiti wa watu,” alisema Mbowe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles