MBOWE AONDOLEWA MASHINE YA KUPUMULIA

0
904

Na Upendo Mosha, Moshi

Hali ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aliyelazwa katika Hospitali ya KCMC inaendelea vizuri baada ya kuondolewa mashine ya Oskijeni.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha hivyo ambapo amesema kwa sasa anapumua mwenyewe bila msaada wa mashine hiyo.

Mbowe alifikishwa hospitalini hapo akiambatana na baadhi ya makada wa chama hicho saa 10:30 jioni jana Jumapili Machi 4, akiwa katika hali mbaya.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema, amesema Mbowe alianza kuugua gafla wakati akipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Tulikuwa tukipata chakula cha mchana katika Hoteli ya Keys lakini Mwenyekiti alisema anajisikia vibaya na afya yake haiko sawa hivyo akataka tumpeleke hosptali ya KCMC kwa ajili ya kuangalia afya yake zaidi.

“Baada ya kumfikisha hosptalini hapo madaktari bingwa walimpima afya yake na kumtaka kubaki chini ya uangalizi wa madaktari kwa matibabu zaidi,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here