33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE AMFUNGULIA KESI MKUU WA WILAYA HAI

Na UPENDO MOSHA-MOSHI


KAMPUNI ya Kilimanjaro Veggies Ltd inayomilikiwa na Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imefungua kesi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa.

Imefungua kesi hiyo dhidi ya mkuu huyo wa wilaya kwa kuwa ndiye anayedaiwa kushiriki uharibifu wa miundombinu ya shamba la mbogamboga inalolimiliki wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Kesi hiyo ambayo iko chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Aishael Sumari, ilifunguliwa Juni 30, mwaka huu na Kampuni ya Uwakili ya D’ Souza& co ya jijini Arusha kwa niaba ya kampuni hiyo.

Kesi hiyo ina mashauri mawili ambayo ni shauri la ardhi namba 20/2017 na maombi madogo namba 51/2017.

Maombi hayo madogo namba 51/2017, yaliletwa kwa hati ya dharura ambapo mdai anaomba zuio la muda liweze kutolewa dhidi ya mdaiwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hai asiweze kufanya chochote katika eneo la shamba la hekari 2.7 lililopo katika Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, katika kesi hiyo, madai ya msingi ni zuio dhidi ya mdaiwa na wafanyakazi au mtu yeyote asiweze kuingilia eneo husika, mdaiwa aombe radhi kwa vitendo alivyovifanya ikiwa ni pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 549.3 kama hasara aliyoipata mlalamikaji.

Mashauri hayo yamepangwa kusikilizwa Julai 13, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles