27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBOWE ALALAMIKA KUNYANG’ANYWA GARI LA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amesema amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge ambalo ni haki yake kuwa nalo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 4, Mbowe amesema amenyang’anywa gari hilo tangu Januari, mwaka huu.

“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.

“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” amesema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.

“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” amesema Kagaigai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles