29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Mbio za magari, pikipiki kutimua vumbi Julai 7 Dar

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

Mashindano ya mbio za magari na pikipiki yanatarajiwa kutimua vumbi Julai 7, 2021, Kawe, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kurudisha mchezo huo katika chati.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa klabu ya mbio za magari ya Mzizima Motorsports, Dennis Rugemalila Rugemalila amesema kwa muda mrefu hawajafanya mashindano kutokana na changamoto za Covid-19.

“Tumerudi tena mashindano ya tarehe saba, yatakuwa ya kwanza kwa mwaka 2021, tumejaribu kuboresha ili kufanya watu wengi wahamasike kupenda mchezo huu.

“Tutakuwa tunashirikisha washiriki wenye magari maalum ya mchezo na binafsi, pamoja na pikipiki. Mashindano yatakuwa ya kilomita 2.2,” amesema Rugemalila.

Kwa upande wake mlezi wa klabu hiyo,Wedson Mwakalundwa, amesema sheria zote zitazingatiwa na washindi watazawadiwa vikombe.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles