MBINU ZA SIMBA KATIKA UWINDAJI, WANYAMA ANAOWAOGOPA

0
3526

Na Edson Ngogo,

WIKI iliyopita tulimzungumzia samba kwa ujumla, ambapo pamoja na mambo mengine tulisema kuwa ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, ukiondolea mbali kwamba ndiye mnyama mkubwa anayewinda katika jamii yao hiyo, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi kwa makundi makundi.

Leo tutaangalia mbinu wanazozitumia katika uwindaji na wanyama wanaoogopwa na simba.

 1. Ni mnyama anayewinda kwa kutumia akili nyingi.
 2. Ni ngumu kumuona awapo katika mawindo hasa hasa kiumbe anayewindwa.
 1. Hana papara anapowinda na hutumia mahesabu makali, kwanza hutambua udhaifu wa anayemuwinda na baada ya hapo shughuli yake huanza, kama mnyama anayemuhitaji anauwezo mkubwa wa kunusa basi atacheza na upepo, kama anayemuwinda ana uwezo wa kuona mbali basi atajificha kwa ustadi.
 1. Ni mnyama asiye na tamaa, anapopanga kukamata windo hubaki na msimamo kwa aliyemteua hata kama kuna nafasi ya kumkamata mwingine, hii ni kwa sababu huofia kuharibu mahesabu ya washirika alionao katika mawindo.
 1. Ni mkatili kwani kabla ya kumkamata anayemuwinda cha kwanza anachokifanya ni kumuharibu kisaikolojia, hali ya kuchanganyikiwa inapojitokeza ndio humshughulikia.
 1. Akiruka juu anapotua huongezeka uzito mara dufu, hufikia karibu kilo 300 sawa na mifuko sita ya saruji utupiwe kwa mpigo.
 1. Tofauti na anapowawinda wanyama wengine akikuona mwanadamu huja kwa spidi huku mgongo wake akiupindisha kushuka chini, hufanya hivi kwa kujihami na hufunga breki kali lengo likiwa ni kukudhoofisha kwa hofu.
 1. Miguu yake ya mbele pia huitumia kama silaha na humsaidia kukamata windo lake hasa anapokimbiza na akatambua kuna ujanja wa chenga unataka kufanyika.

SIFA ZAKE ZA KUSTAAJABISHA 

 1. Anapowinda unyayo wake huwa haugusi chini.
 2. Simba ni mnyama mvivu asiye na mfano, hutumia muda wake mwingi kupumzika hata kama hajachoka, takribani saa 15 hadi 20 katika saa 24 hutumia kubadilisha mapozi tu.
 3. Pamoja na ukali wake wote lakini cha ajabu mnyama fisi ana uwezo wa kumnyang’anya chakula alichowinda.
 4. Anapokula hapendi kabisa kukerwa hivyo zikitokea kelele au harufu ambayo itamkera yupo tayari kuacha nyama na kwenda zake.
 5. Hali nyama ambayo hajawinda mwenyewe.
 6. Ni mnyama ambaye anajiamini na anajijua kwamba anaogopwa.
 7. Ana uwezo mkubwa wa kuona mbali, ikiwa ni pamoja na kusikia, uwezo wake humsaidia kuwinda wakati wowote ule anaojisikia iwe usiku au mchana.
 8. Ili kutengeneza mimba dume na jike hukutana mara nyingi na mara zote jike huwa anatembea tembea ili kubadili mazingira huku akimpiga piga dume na mkia wake. Dume anapompanda wanapohitimisha tendo hilo jike humfukuza kwa kuunguruma na anapotoka jike hujiangusha kwa ubavu mmoja, huku dume likitazama huku na kule, baada ya muda mfupi hurudia zoezi hilo tena kama walivyoanza awali.
 9. Wanapomaliza tendo huwa wakali zaidi na ni hatari mara dufu kuwasogelea kwani wanaweza kufanya chochote.

10. Licha ya kwamba simba hujipatia kitoweo chake kwa urahisi, lakini baadhi ya wanyama humpa tabu akiwamo nyati, kuna wakati wakichachamaa huweza hata kumuua simba asipowaingia kwa akili mkubwa.

Pundamilia naye hutumia vyema miguu yake ya nyuma kwa kukimbia pia kama silaha, simba wengi hupata majeraha yanayosababishwa na wanyama hawa.

Licha ya kwamba simba ni hatari, lakini hushindwa kuwaangusha hata tembo wadogo hata wao wakiwa zaidi ya watano.

 1. Simba huua pale anapojisikia njaa tu, vinginevyo ni kama amehisi kuna hatari ambayo inaweza jitokeza.

Pamoja na yote unachotakiwa kujua simba ni mnyama hatari na wa kuogopwa zaidi ya neno lenyewe, kwani mnyama huyu huwa na tabia ya kuua mara mbili, kabla ya kukuua kwa kukurarua, anakuwa tayari ameshakuua kwa hofu, kwa Tanzania karibia mbuga zetu zote zina simba, unaweza kutembelea mojawapo ujifunze mengi juu ya wanyama hawa.

Kwa Leo naomba niishie hapa karibu kwa maoni. Pia unaweza kushauri mnyama unayehitaji tumzungumzie wiki ijayo.

Wasiliana nami kwa namba 0715202047.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here