27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MBINU ZA AJABU ZA KUZUIA UDANGANYIFU WA MITIHANI

mitihaniKILA mtu amepitia shule achilia mbali wenzetu wachache, ambao kwa sababu moja au nyingine hawakubahatisha kupitia maisha ya darasani.

Katika hilo wengi tulioonja elimu rasmi ya darasani suala la udanganyifu wa mitihani si geni bali ni sehemu ya utamaduni katika taasisi zetu za elimu kuanzia ngazi za chini hadi chuo kikuu.

Mbinu za udanganyifu ni nyingi mno na huweza kufanana au kutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine lakini kuna ubunifu mpya unaoweza kukuacha kinywa wazi usiamini kama kuna watu wanaoweza kubuni aina hiyo ya wizi.

Utakuta mtu badala ya kuumiza kichwa kuzama kitabuni, anatumia muda mwingi kubuni mbinu mpya za udanganyifu ambazo hazitaweza kushtukiwa na wasimamizi.

Lakini tatizo hili halipo katika taasisi zetu za elimu tu bali kote duniani.

Mbinu zinazotumiwa na wanafunzi wa mataifa mengine ni kali zaidi zikihusisha pamoja na mambo mengine matumizi ya teknolojia mpya.

Kwa sababu hii ya teknolojia katika zama hizi, tatizo linazidi kukua siku hadi siku likihusisha vitu mbalimbali kama vile saa, miwani, vitu vya kuchomeka kwenye masikio ili kuwasiliana na mtu wa nje ya chumba cha mtihani na kadhalika.

Ili kujaribu kuiokoa elimu, mamlaka husika shuleni au vyuoni wamekuwa wakikuna vichwa kuja na mbinu mbalimbali za kudhibiti tatizo hilo zikiwamo zinazoweza kuwa haramu.

Miongoni mwao ni zile zilizotumiwa na Chuo cha Thomas More huko Antwerp, Ubelgiji, ambako walimu walilazimika kutumia drone zenye kamera kukamata wanafunzi wanaojaribu kufanya udanganyifu katika mitihani.

Nchini India katika jimbo la Bahir mapema mwaka huu, habari zilizoteka vyombo vya habari duniani ni tukio la waombaji waliotaka kujiunga na jeshi kulazimishwa kuvua nguo zao na kubaki watupu. Wasimamizi walikuwa na matumaini kuwa mpango huo hautaruhusu yeyote kudanganya kwa kuingiza kwa siri karatasi au kifaa chochote cha kielektroniki au kuondoa uwezekano wa kuwa na maandishi mwilini.

Baada ya kubaki watupu wanafunzi 1,159 walikaa umbali wa futi nane kutoka mmoja baada ya mwingine huku askari wenye sare wakifanya doria wakati wanafunzi wakifanya mtihani huo wa saa moja.

Aidha mwaka 2013, katika Chuo cha Ualimu Kasetsart nchini Thailand, kilipigiwa kelele kwa kuwalazimisha wanafunzi wao kuvaa kitu kinachofanana na kinga macho za farasi (horse blinder) kilichotengenezwa na karatasi ili kuwazuia kuangalia pembeni na kufanya undanganyifu wowote.

Picha iliyoonesha wanafunzi 100 wakiwa wamevaa kofia zinazozuia kuona iliwekwa katika ukurasa wa Facebook wa mwanafunzi wa chuo hicho, lakini ilipokelewa vibaya hali iliyosababisha kuondolewa mara moja baada ya kuonekana kuidhallisha taasisi hiyo ya elimu ya juu.

Lakini bahati mbaya sana ilichelewa kuchukua hatua kwani ilishatekwa na vyombo vya habari.

Wanafunzi zaidi ya milioni nane wa China hukusanywa katika chumba kikubwa cha mitihani ambako hufuatiliwa kwa chati na kamera mbalimbali zilizojazana kila mahali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la China (Xinhua) limeeleza kwamba kitendo hicho kinaifanya kuwa moja ya mitihani yenye shinikizo zaidi duniani.

Pia China inajulikana kama kiongozi wa kutumia vifaa mbalimbali vya kiteknolojia kuzuia udanganyifu katika mitihani.

Picha zifuatazo zinaeleza mbinu mbalimbali zinazoweza kukuacha mdomo wazi za kuzuia udanganyifu katika mitihani ambazo baadhi zimeshaelezwa kwa ufupi hapo juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles