27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

MBILIKIMO ANAYEJIHISI MWENYE BAHATI KUTOKA NA MSICHANA MREFU

KAMA mwanamume pekee duniani mwenye uwezo wa kunyanyua vitu vizito mara nne wa uzito wake mwenyewe, Anton Kraft, linapokujua suala la ‘uzito kwa uzito’ ni mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Mbilikimo huyo mwenye urefu wa futi 4'4', mkazi wa Florida, ameweza kuinua uzito wa stone 36 sawa na kilo 229.

Kraft , 52, hupenda kutoka na wasichana wenye urefu mkubwa zaidi ya wake na kwa miezi sita iliyopita amekuwa akitoka na China Bell mwenye urefu wa futi 6'3'.

Bell (43), ambaye alizaliwa mwanamume kabla ya kubadili jinsia kuwa  mwanamke, alipoombwa uhusiano na jamaa huyo mwenye nguvu, haraka haraka alijikuta akimkubalia kutokana na kulewa na ujuzi wake wa kunyanyua vitu vizito.

“Nadhani unyanyuaji wa vitu vizito wa Anton umenivutia  mno, lakini pia kwa sababu yeye mwenyewe anavutia pia, wakati unaposhikilia taji la unyanyuaji wa uzito wa juu duniani huwa unamaanisha mengi,” Bell anasema.

“Kamwe nilikuwa sijawahi kutoka na mpenzi mwenye urefu wa futi 4'4", lakini nilikuwa na shauku nilipokutana naye. Nina furaha nimempata kwa bahati kwa sababu yeye yu mtu wa aina yake.

Mimi niko tofauti naye yu tofauti na tunakotoka, tofauti ni nzuri.

Miaka 10 ya kunyanyua vitu vizito, Kraft anadai kuwa na rekodi ya wakati wote kwa daraja lake la uzito.

Lakini inaonekana amezidisha kipimo cha kunyanyua uzito zaidi ya mwili wake.

Anasema ‘kiufundi amekufa’ mara tano kabla ya kufufuka – kutokana na kukumbana na matukio kuanzia kusombwa na mafuriko hadi kuanguka kutokea dirishani.

Madaktari wana wasiwasi kuwa  huenda akapata shambulio la moyo iwapo ataendelea na mfumo wake wa maisha hayo ya unyanyuzi wa vitu vizito visivyoendana na ule wake.

Lakini Kraft haonekani kubabaishwa na hilo.

“Baadhi ya watu wanasema ninachofanya ni udhaifu, lakini nataka kufanya kitu ambacho sina, ninachoweza kuthibitisha kuwa nakiweza.”

“Kwa ujumla mimi ni mmoja wa watu watano wenye nguvu zaidi duniani bila kujali urefu na uzito.

“Na zaidi mimi ni mwanamume pekee duniani kuwahi kunyanyua uzito mara nne zaidi ya ule wa mwili wangu,” anajigamba.

Anayemtia nguvu katika harakati zake hizo, anasema ni rafiki wake huyo wa kike. 

“Florida ni moja ya majimbo yenye ndoa za jinsia moja na sote kimsingi ni wa watu jinsia moja.

“Nafurahia kutoka na mwanamke aliyebadili jinsia kwa sababu alizaliwa mwanaume akaweza kufanya kila linalowezekana kuwa mwanamke.

“Nakutana na sehemu kubwa ya wanawake, ambao wamezaliwa wakiwa wanawake, ambao hata hivyo, sina muda mwingi wa kushughulika nao.

“Kwa sasa kwa mafanikio yangu ukiongeza na kuwa na mpenzi nimpendae wa aina hii, hakika najihisi kuwa mwanaume mwenye bahati kuliko wote duniani.

“Hakika tuna furaha sana na ukweli najisikia vyema kuliko kipindi chote cha maisha yangu. Shukrani hakika zimwendee China,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles