25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mbelgiji Yanga achekelea ushindi wa kwanza VPL

Theresia Gasper-Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema amefurahi kuona wachezaji wake wakifanya kile alichowaelekeza na kupata pointi tatu muhimu katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United, uliochezwa juzi Uwanja wa Liti Singida.

Yanga juzi ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United na kuwafurahisha mashabiki wake.

Ushindi huo ni wa kwanza tangu Eymael atue Yanga ambako wamepoteza mechi mbili mfululizo ikiwa dhidi ya Kagera Sugar 3-0 na Azam FC 1-0, katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo Eymael alisema washambuliaji wake walipata nafasi nyingi za kufunga ila walizitumia tatu na kuifanya timu hiyo ivune pointi tatu muhimu.

“Tumeweza kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo huu baada ya kupoteza michezo miwili nyuma, hii ni kutokana na kuingia na mbinu mpya iliyowapoteza wapinzani wetu na kuwazidi,” alisema.

Alisema kwa sasa wanarejea nyumbani kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kuchezwa Januari 26 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Eymael alisema kwa sasa hawatakubali kufanya makosa mengine kirahisi kwani wanahitaji kujituma na kupata kile ambacho wanahitaji katika mechi zao.

Ushindi huo umeipandisha Yanga hadi nafasi ya nne baada ya kucheza michezo 15 na kujikusanyia pointi 28 wakipoteza mara tatu na kutoa sare nne huku wakishinda mechi nane.

@@@@@@@@@

Mghana Yanga afunguka kiwango chake

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa Yanga, Benard Morrison, ameweka wazi kuwa mpira hauna ugeni na unapopata nafasi ya kucheza lazima uonyeshe uwezo wako hadi mwisho ili kuipatia timu yako matokeo.

Morrison juzi alicheza mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe na Yanga wakati wa dirisha dogo akitokea Motema Pembe ya Congo, katika mchezo dhidi ya Singida United ambao ulimalizika kwa timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Liti, Singida.

Kwenye mchezo huo Morrison aliweza kuonyesha makeke ikiwa ni pamoja na kutengeneza kupatikana kwa mabao mawili yaliyofungwa na David Molinga na Haruna Niyonzima.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Morrison alisema ilikuwa ni lazima wapate matokeo kutokana na kupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi.

“Mpira unachezwa wazi na hauna ugeni hivyo pale unapopata nafasi ya kucheza lazima uonyeshe uwezo wako wote ili kuisaidia timu ipate matokeo ukizingatia tumetoka kupoteza,” alisema.

Alisema ushindi waliopata umerudisha furaha kwa mashabiki pamoja na benchi la ufundi ambako kwa sasa wataendelea kupambana kwa mechi zinazowakabili mbele yao.

Morrison alisema wataendelea kuwa makini katika mechi zinazowakabili ili wapate matokeo mazuri na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles