25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbelgiji: Msihofu Simba itafuzu robo fainali

SOSTHENES NYONI-DAR ES SALAAM

 KOCHA wa Simba, Mbelgiji amesema ana imani kikosi chake kina uwezo wa kupambana na kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), juzi lilichezesha droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Simba ilipangwa kundi D pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vital ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na JS Saoura ya Algeria.

Wekundu hao watazindua kampeni zao za hatua hiyo nyumbani Januari 11 kwa kuumana na J.S. Saoura kabla ya kuifuata AS Vita Januari 18 mjini Kinshasa na Al Ahly Februari 1 jijini Cairo kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems, alisema ana imani na ubora wa kikosi chake kwamba kinaweza kupambana na wapinzani wao katika kundi D na kufuzu robo fainali.

“Kundi lipo wazi  kwa timu yeyote kusonga mbele, kwa upande wetu  naamini tuna kikosi  kinachoweza kushindana na mpinzani yeyote na kupata ushindi.

“Jambo la msingi ni kuunganisha nguvu kwa pamoja kuanzia benchi la ufundi, uongozi na mashabiki ili kuhakikisha azma yetu inafikiwa,” alisema Aussems.

Simba imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 13, mara ya mwisho ilifanya hivyo mwaka 2003 ilipoitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 3-2, baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani.

Lakini safari hii imefuzu kwa kuitoa Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3, ikichapwa mabao 2-1 ugenini mjini Kitwe kabla ya kushinda mabao 3-1 nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles