31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbatia aitaka Serikali iwe na taasisi imara kukabili majanga

NA ASHA BANI -DAR ES SALAAM

MWENYEKITI Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameishauri Serikali kuweka taasisi au mamlaka ya kuweza kusimamia kwa ukaribu masuala ya majanga yanayotokea nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na mvua zilizosababisha mafuriko na watu kadhaa kupoteza maisha.

“Majanga yanayoendelea kutokea maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya mvua, mengi yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Ambapo zaidi ya asilimia 96 ya majanga yanasababishwa na binadamu wenyewe,’’ alisema Mbatia.

Aidha alisema sheria ya mwaka 2015 walishauri kuwepo na mamlaka kamili ya kukabiliana na majanga hayo na inatakiwa kusema ni lazima isimamie majanga yote na iwe inachukua hatua haraka.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alisema kuwa suala la maafa ni suala la kitaalamu, hivyo mamlaka hiyo ikiundwa inakuwa na wataalamu maalumu ambao watakuwa maalum kwa kusimamia majanga hayo.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimesema kuwa kimejipanga kuweka wagombea ngazi zote katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Mbatia alisema kuwa katika kikao cha Kamati ya Halmashauri Kuu ya Taifa walichokifanya juzi, kwa pamoja wamekubaliana watashiriki uchaguzi wa Oktoba kwenye ngazi zote.

Alisema Februari 19, mwaka huu wameitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Dar es Salaam kujadili mikakati ya pamoja na kuweza kutoa ratiba ya ndani ya chama namna ya kujiandaa kushiriki kikamilifu Uchaguzi Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles