27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

MBARONI KWA WIZI WA MAFUTA YA NDEGE

Na HERIETH FAUSTINE – Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya  Dar es Salaam, linamshikilia Iddy Nyangasa (42), mkazi wa Buguruni Mnyamani kwa tuhuma za kuiba lita 40 za mafuta ya ndege, mali ya Kampuni Ndege ya Tanzania (ATCL).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalumu,  Kamishna Simon Sirro, alisema  Machi 17,mwaka huu, saa 6:30 usiku katika hanga la Kampuni ya ATCL, maofisa wa usalama wa uwanjani hapo walimkamata Nyangasa ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya Moku, akiwa na lita 40 za mafuta ya ndege toka kwenye ndege yenye namba za usajili 5H-MWF aina ya DASH 8,Q300.

Alisema kuwa  ndege hiyo ilikuwa katika hanga la ATCL kwa ajili ya matengenezo.

“Baada ya kukamatwa ndipo ilibainika kuwepo kwa mtandao wa wizi wa mafuta ya ndege ambao pia unahusisha askari polisi wawili wa kikosi cha anga ambao ni F.8419 CPL Bahati Msilimi na F.9901 PC Benau Mkama.

“Askari hao wamekamatwa kwa uchunguzi zaidi na mara utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Kamishna Sirro.

Alisema kuwa baada ya ukaguzi wa kina wahandisi wa ATCL waligundua jumla ya lita 220 ziliibiwa toka katika ndege hiyo.

Alisema, wizi wa mafuta ya ndege ni hatari sana, kwani unaweza kusababisha janga kubwa la moto au ajali kwa ndege kwa kukosa mafuta na imebainika kuwa mafuta hayo  yamekuwa yakiuzwa kama mafuta ya taa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles