23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa unyang’anyi wa silaa

Na AVELINE KITOMARY

DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es salaam imempandisha kizimbani Ernest Benedict (19) Mkazi wa Mburahati kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Mwendesha mashtaka wa Jamuhuri Neema Moshi alidai mnamo Machi 17 mwaka huu eneo la Mburahati National Housing, Wilaya ya Kinondoni mtuhumiwa aliiba simu aina ya Samsung J7 yenye thamani ya Sh 380,000 mali ya Amina Said,kabla na baada ya kuiba alimtishia kwa kisu Amina Said na Hamadi Shante ili kujipatia mali hiyo.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Kutokana na shtaka hilo kutokuwa na dhamana kisheria mshtakiwa alirudishwa rumande mpaka kesi yake itakaposomwa tena Mei 20 mwaka huu.

Wakati huo huo Mahakama imempandisha kizimbani Raymond William  (44)  Mkazi wa Kinondoni  kwa shtaka la wizi wa gari.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, Mwendesha mashtaka wa Jamuhuri Ester Charles alidai katika tarehe isiyojulikana Disemba mwaka 2017 eneo la Mabibo Wilaya ya Kinondoni mtuhumiwa aliiba gari lenye namba za usajili T. 137 AWQ aina ya Noah yenye thamani ya Sh. Milioni 8.5 mali ya Rodrick Emily Mayani  aliyopewa na Gibson Mayani kwaajili ya kulitengeneza.

Mtuhumiwa alikana kufanya kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mushi alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka katika taasisi inayotambulika kisheria watakaotoa bondi ya Sh millioni 1 kwa kila mdhamini mmoja.

Hata hivyo Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka shauri hilo litakaposikilizwa tena Mei 13 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles