27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa tuhuma za kumpa mwanafunzi mimba

Na, MALIMA LUBASHA, SERENGETI.

JESHI la Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara, linamshikilia Wambura Sukuru (34) mkazi wa Mugumu kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wa shule msingi  wakati wa likizo ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona.

Mkuu Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alithibitisha kuwapo tukio hilo alipozungumza na MTANZANIA ofisini kwake kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu watu wanaotuhumiwa kuwapa ujauzito wanafunzi wa shule za msingi na sekondari .

Alisema mwanafunzi (jina tunalo), anayesoma Shule ya Msingi Kambarage Kata ya Stendi Kuu wilayani, ni mjamzito kukutokana na kuwa na uhusiano na Sukuru.

Alisema mwanafunzi huyo, ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 20 wa shule za msingi na sekondari  waliothibitishwa na idara ya elimu kupewa mimba kipindi wakiwa nyumbani  wakati wa likizo ya corona, hali ambayo imekatisha ndoto za watoto hao kuendelezwa kielimu.

Alisema taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa zinaendelea na kuwaonya watu wote wanaoshawishi watoto wa kike kujihusisha na vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo.

Alisema ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu wa afya pamoja na vyombo vya usalama wanaendelea kufanya ufuatiliaji kubaini hali ya afya ya wanafunzi wote  wa kike, baada ya likizo ya corona ili watakaobainika kuwa na ujauzito uchunguzi wa watuhumiwa ufanyike haraka iwezekanvyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles