27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa mtandao wa dawa za kulevya

siroASIFIWE GEORGE NA MARTHA LUKUMAY, DAR ES SALAAM

JESHI la Polis Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa kuuza dawa za kulevya, huku wakiendelea kumuhoji mtuhumiwa mwingine kwa tuhuma hizo hizo.

Akizungumza jijini hapa jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simon Sirro, alisema watuhumiwa hao ni miongoni mwa wauza dawa wazoefu na walitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka yanayowakabili.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa na kilogramu tisa za dawa za kulevya aina ya heroine kutoka nchini Pakistan.
Aliwataja watuhumiwa hao wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuuza dawa za kulevya kuwa ni pamoja, Mohamed Omari (37) mkazi wa Tegeta Nyuki anayetuhumiwa kwa kusafirisha dawa hizo na usafirishaji haramu wa binadamu.

“Huyu mtu anatuhumiwa kwa kumsafirisha mtu ajulikanae kwa jina la Mwinyi Mgobanya mkazi wa Ununio na kumuweka rehani huko Pakistan kisha akachukua dawa za kulevya kwa mali kauli,” alisema Kamanda Sirro.

Alimtaja mtuhumiwa mwingine ni Nassoro Suleiman ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Tungwe Bureau De Change iliyopo katika Jengo la IPS jijini Dar es Salaam ambaye anatuhumiwa kushirikiana na genge ka wauzaji wa dawa za kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha kwa njia zisizo rasmi.

Kamanda Sirro alimtaja myihimiwa mwingine ni Daudi Adam (46) mfanyabiashara mkazi wa Salasala na Kibaha ambaye anaendelea kuhojiwa.

Akizungumzia kuhusu takwimu za mwaka 2014 alisema zinaonyesha kilogramu 304.91 za heroine na kilogramu 68 za cocaine zilikamatwa pamoja na watuhumiwa 14,501 ambapo miongoni mwao Watanzania walikuwa 14,467 ikilinganishwa na mwaka 2010 ambapo zilikamatwa kilogramu 123 za heroine.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro alisema Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata magari manne yaliyokuwa yameibwa maeneo tofauti ya Dar es Salaam na mikoani.

Alimtaja John Samwel mkazi wa Mwanjelwa mkoani Mbeya kwamba alikamatwa kwa wizi wa gari aina ya Toyota IST, rangi nyeusi T 271 DCT iliyoibiwa nyumbani kwa Dk. Reginald huko Kimara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles