23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

MBARONI KWA MENO YA TEMBO

 JESHI la polisi mkoani Simiyu linamshikilia Kimola Salulu (30) wa Kijiji cha Mwakiloba katika Kata ya Lamadi wilayani Busega   kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili yanayodhaniwa kuwa ya tembo, anaripoti Derick Milton.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Jonathan Shana alisema   mtuhumiwa huyo alikamatwa kijijini hapo Machi 19 mwaka huu   na  polisi waliokuwa kwenye doria maalum ya kupambana na ujangili ndani ya hifadhi.

Alisema  katika operesheni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,   nyara hizo zilikamatwa   nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles