24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mbaroni kwa kutakatisha Sh milioni 15 akitumia jina la mke wa Rais Magufuli

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

WAFANYABIASHA wawili wakazi wa jijini la Dar es Salaam, wanaotuhumiwa kutumia jina la mke wa Rais, Janeth Magufuli kutapeli, wameshtakiwa kwa kujipatia Sh milioni kwa udanganyifu na utakatishaji fedha.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augutina Mmbando na kusomewa mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga na Wankyo Simon.

Washtakiwa hao ni mkazi wa Tegeta Wazo, Nkinda Shekalaghe (34) na mkazi wa Kitunda Magore, Masse Uledi (43).

Akiwasomea watuhumiwa mashitaka yao, Wakili Mshanga alidai kati ya Januari na Machi 31, mwaka huu kupitia mtandao wa Facebook watuhumiwa walichapisha habari iliyosema “Janet Magufuli  Saccos’ mpya 

isome tafadhali, mkopo yote ni online tuu! Na utaupata ndani ya dakika 45 tu, mikopo huanza kutolewa kuanzia 300,000 hadi 20,000 fuata utaratibu huu ili kupata mkopo.

“Tuma namba za kitambulisho chako cha mpiga kura au Nida (Kitambulisho cha Taifa) na majina yako matatu kupitia namba hii 0685012921 kisha piga namba hiyo ili upatiwe namba ya mhasibu ili kuweka akiba hatimaye kupata mkopo.” Alisema watuhumiwa walifanya hivyo huku wakijua ni uongo.

Katika shtaka la pili alidai, watuhumiwa wanadaiwa kati ya Januari na Machi 31, mwaka huu kwa pamoja walitoa taarifa za uongo na kujipatia miamala ya Sh. 15,068,650 kwa njia ya simu kutoka mahali tofauti na kwa watu tofauti.

Wankyo alidai katika shtaka la tatu, kati ya Januari na Machi 31, mwaka huu mahali tofauti nchini walitakatisha fedha hizo huku wakijua ni kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi.

Kesi hiyo iliahirishwa na itatajwa Aprili 30,mwaka huu, washtakiwa wamepelekwa mahabusu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles