25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kulipa mamilioni ya Tasaf marehemu

Safina Sarwatt-Hai

WARATIBU tisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) Wilaya Hai, wamekamatwa na kuwekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuwalipa wanufaika hewa 1,045 na kusababishia Serikali hasara ya Sh milioni 324 kwa mwaka.

Kukamatwa kwa waratibu hao kumefuatia taarifa ya  uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai ole Sabaya, kuchunguza mienendo na undeshaji wa mfuko huo.

Taarifa ya kamati hiyo iliyowasilishwa na Katibu wa kamati ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Hai, Englberth Kalekona, ilisema kamati imebaini kati ya watu waliodaiwa kupewa fedha hizo, 193 walikwishafariki dunia, lakini wanaendelea kulipwa na 516 ni hewa, lakini wako kwenye orodha ya wanufaika wa Tasaf.

Kalekona alisema kuwa kamati hiyo pia imebaini watu 324 ambao hawastahili kuingizwa kwenye mpango huo wa kaya masikini.

Alisema miongoni mwa watu hao wengine ni watumishi wa umma, wastaafu ambao wanapokea mafao, madiwani wawili na baadhi yao ni wafanyabiashara na wenyeviti wa vijiji na wengine hawapo kabisa.

Kalekona alisema kamati hiyo imebaini wanufaika ambao wanastahili kulipwa fedha za Tasaf ni 3,887 .

Kutokana na hali hiyo, Sabaya alitangaza kuvunja kamati zote za Tasaf za wilaya na vijiji kutokana na kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 44.5 kwa mwezi na Sh. milioni 324 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles