23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kukutwa na nyara za serikali

Na BEATRICE MOSSES-MANYARA

WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, baada ya kukamatwa wakiwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Akisoma kesi hiyo mwendesha mashtaka wa Mamlaka ya ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Timoth Mmary, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Neema Mmary, alisema watuhumiwa wanakabiliwa na makosa mawili.

Mmary aliwataja washtakiwa kuwa ni Ally Bakari (35) mkazi wa Kolang’a Kilindi na  Bakari Mwinjuma (61) mkazi wa Kikwembe Kilindi.

Alisema katika kosa la kwanza, watuhumiwa kwa washtakiwa wote wawili walikutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Maelezo ya kosa Mmary alisema Juni 9, mwaka huu katika eneo la Kitwai Wilayani Simanjiro, walikutwa na nyara za serikali ambayo ni nyama ya Tandala mdogo yenye thamani ya Sh milioni 5,480,000 mali ya serikali pasipo kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kosa la pili ni kupatikana na silaha kinyume cha sheria ambapo Ally Bakari Zahoro na Bakari Mwinjuma Kilonga ambapo Juni 9, mwaka huu  katika maeneo ya Kitwai Wilaya ya Simanjiro, walikutwa na silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya gobole pasipo kuwa na kibali kutoka kwa msajili wa silaha.

Hakimu Gasabile, aliwaambia washtakiwa wote wawili kuwammeyasikia mashtaka wanayoshtakiwa nayo na mahakama haina mamlaka hivyo hamtapaswa kujibu chochote kile.

Mmary alisema upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuomba tarehe ya kutajwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Jului 4, mwaka huu itakapotajwa tena.

Wakati huo huo mtu mmoja amefikishwa mahakamani kwa makosa matatu ambapo kosa la kwanza ni kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Akisoma kesi hiyo mwendesha mashtaka wa Tanapa, Linus Bugaba mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, Neema Bugaba, alisema katika kosa la kwanza mshtakiwa Mkomwa Athman Mkumpehe (70) mkazi wa Kikwembe Kilindi.

Alisema Jun 8, mwaka huu katika pori tengefu la Kitwai lililopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mshtakiwa alipatikana na fuvu moja la Simba na gamba moja la Kakakuona ambavyo vina thamani ya Sh milioni 13,478,000 mali ya serikali bila kuwa na kibali kutoka wa Mkurugenzi wa Hifadhi ya Wanyamapori.

Kosa la pili ni kupatikana na pembe moja ya Pofu, fuvu la Nguruwe pori, fuvu la Kuro pamoja na fuvu moja la Mbweha wa dhahabu ambapo vyote kwa pamoja thamani yake ni Sh milioni 7,544,000 mali ya serikali bila kuwa na kibali toka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori.

Na kosa la tatu ni kupatikana na silaha moja aina ya bunduki   ijulikanayo kama gobole pasipokuwa na kibali toka kwa msajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,183FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles