24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaroni kwa kuiba transfoma ya Tanesco

Na Nyemo Malecela-Kagera

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amesema wamekamata watu wawili wakaazi wa Arusha kwa tuhuma za kuiba transformer katika Kijiji cha Kabukome wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wakijifanya kuwa ni mashundi wa Shirika la Umeme (Tanesco).

Watuhumiwa hao ambao ni Frank Muneja (38) mfanyabiashara wa Arusha na Athuman Sabuni (37), ambao walikamatwa Machi 5 mwaka huu  wakiwa na transformer hiyo ikiwa kwenye gari aina ya Nissan Hard body pickup kwenye barabara itokayo Biharamulo kwenda Lusahunga mkoani Kagera.

Kamanda wa Malimi alisema transformer waliyokutwa nayo namba TX 011623/2019 50KVA/33KVA mali ya TANESCO yenye thamani ya Sh 8,000,000.

“Walijifanya ni wafanyakazi wa TANESCO wa fani ya na walikuwa wanaenda kuifanyia matengenezo hiyo transformer.

“Jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi waliowashtukia watu hao ambao walikuwa wanne, tuliwafuatilia na kufanikiwa kuwakamata,” alisema Malimi.

Katika mahojihano watuhumiwa hao ambao walikuwa wanne waligundulika hawakuwa watumishi wa TANESCO na wawili walitoroka.

“Sabuni ambaye ni fundi wa kutengeneza transformer na kampuni wa kampuni ya Sahali Electrical Service Company LTD yenye makao yake Arusha mjini alidai ana mkataba na Shirika la Tanesco Tanzania wa kufanya huduma za ufundi transformer nchi nzima.

Alidai walipigiwa simu na kandarasi wa mradi wa REA eneo hilo waje kuichukua transformer hiyo kwenda kuifanyia matengenezo,” alisema Malimi.

Alisema kwa mujibu wa maofisa wa Tanesco, transformer hiyo si mbovu kwani ndio kwanza imefungwa na haijaanza kupokea umeme na kandarasi wa REA anayedaiwa kuwaita hakuhusika na mradi huo wa Tanesco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles