21.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Mbaroni kujifanya ofisa TAKUKURU

Na Tunu Nassor-Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) Mkoa wa Ilala, inamshikilia Mkazi wa Mbagala, Kijiji Dar es Salaam Hussein Mhando kwa kujifanya ofisa wa Taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari’ leo Desemba 19, mwaka huu, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema mtuhumiwa hiyo amegushi na kutengeneza kitambulisho namba PCCB 1565 chenye cheo cha Ofisa Mchunguzi Mkuu(principal investigator) .

Amesema kwa kutumia kitambulisho hicho mtuhumiwa amekuwa akiwatapeli watu na kujipatia kipato kinyume Cha sheria.

“Baada ya kupata taarifa Desemba 12, mwaka huu tulimwekea mtego Mwananyamala, kwa bahati mbaya alikimbia baada ya kuona watu asiowajua na kutelekeza gari lenye namba T618DMS alikitumia siku hiyo.

Amesema Takukuru ililishikilia gari hilo hadi Desemba 16 ambapo mtuhumiwa aliamua kujisalimisha na kukiri kutenda kosa hilo. 

Myava ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa namba 113 pindi wanapobaini kuwapo kwa uhalifu wenye taswira ya rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles