24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mbaroni akituhumiwa kumuua mpwa wake kwa kichapo

Elizabeth Kilindi – Njombe

MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Apronia Mwinuka (35), mkazi wa mtaa wa Kikula, Kata ya Makambako mkoani Njombe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Elina Mwinuka (18) kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitokea kwa mpenzi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah alisema tukio hilo lilitokea Januari 27 saa 11:52 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji Makambako.

Kamanda Issah alisema Elina alitumwa na shangazi yake na kuchelewa kurudi hali iliyosababisha kuanza kumpiga.

‘’Alichokifanya shangazi, aliamua kutoa adhabu ya kipigo kwa binti na kile kipigo kikasababisha akafariki dunia wakati amepelekwa kupata matibabu,’’ alisema Kamanda Issah.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Issah alitoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kuacha kuwapiga watu bila ya kuchukua tahadhari.

“Niwasihi wananchi wa Njombe kuacha tabia ya kupiga watu, mfano huyu shangazi Apronia kampiga shangazi yake na hakuchukua tahadhari yoyote, kampiga mpaka sehemu za kichwani na mwili wa marehemu huyu umeonekana una uvimbe na alivyofikishwa hospitali amefariki.

“Tunawasihi msitoe adhabu zinazopita kikomo, kwa mfano kumpiga mtu, huwezi kujua mtu ana matatizo gani, kama huyu mzazi aliyempiga huyu binti tayari kamsababishia kifo,” alisema Kamanda Issah.

Aidha alisema Jeshi la Polisi linaendelea na taratibu ili kuweza kumfikisha mahakamani Apronia na kwamba kwa sasa marehemu yupo chumba cha maiti akisubiri kufanyiwa uchunguzi na baadae kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Naye mume wa Apronia, Tadei Mhongole alisema tukio hilo limetokea wakati yeye akiwa kwenye shughuli za utafutaji na aliporudi alikuta binti huyo akiwa amezimia baada ya kupigwa na shangazi yake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles