25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MBARAWA ATAKA USALAMA VIWANJA VYA NDEGE

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM



WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametaka usalama katika viwanja vya ndege kushughulikiwa kuepuka tukio kama lilitokea Mwanza ambako mto mmoja alifariki dunia kwa kugongwa na ndege.

Akizungumza Dar es Salaam jana alipozindua baraza jipya la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Mbarawa alisema ni vizuri suala la usalama lipewe kipaumbele katika viwanja vyote nchini.

Hata hivyo aliwataka wanafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea ya kukusanya Sh bilioni 134 kwa mwaka mpya wa fedha unaoanza Julai mosi mwaka huu na ikiwa watashindwa kukufikia lengo hilo wasaharu huhusu kuongezwa mishahara.

“Naamini tukifanya kazi yetu vizuri tutakusanya mapato mengi na mishahara yetu tutapanga tuongeze kiasi gani, hakuna mshahara utakaongezwa kabla hamja-perform,” alisema.

Profesa Mbarawa aliitaka TAA kutotegemea mapato yatokanayo na viwanja moja kwa moja badala yake wahakikishe wanatumia fursa mbalimbali zilizopo kutengeneza faida zaidi.
Hata hivyo alishangazwa na kitendo cha viwanja vya ndege vya Tanzania bara kushindwa kuingia katika orodha ya viwanja 10 bora Afrika.

“Ninyi ndiyo mnaokwenda kuwa kiungo katika ya viongozi na wafanyakazi, hivyo mna jukumu la kuhakikisha huduma zinazotolewa na wafanyakazi wa viwanja vyote vya zinafikia viwango vinavyotakiwa.

Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAA, Richard Mayongela, alisema wamekwisha kuanza kushughulikia suala la usalama katika viwanja mbalimbali vya mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa uzio katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles