27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mbarawa aeleza mwarobaini kukamilisha miradi ya maji, Spika Ndugai akitoa kilio kipya

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, amesema wizara yake itaendelea kutumia force akaunti katika kutekeleza miradi ya maji kwani ndio mwarobaini kwa wakandarasi ambao ni wapigaji, huku Spika Job Ndugai akisema kuna vijiji havijawahi kupata maji hivyo wizara iwaonee huruma wabunge wanaolilia huduma hiyo.

Akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, Profesa Mbarawa alisema wizara yake itaendelea kutumia force akaunti katika kutekeleza miradi yake licha ya kwamba wakandarasi wengi wamekuwa hawaupendi utaratibu huo.

 “Lazima twende na utaratibu wa force akaunti  hakuna namna nyingine, hatusemi miradi yote lakini tunaamini asilimia kubwa tutajenga kwa force akaunti.

 “Hadi sasa wizara inajenga miradi 192 kwa force akaunti gharama ni Sh bilioni  163.77 lakini  kwa kutumia wakandarasi ingekuwa Sh bilioni 250 hadi 300 na ukamilishaji wake ungechukua miaka miwili hadi mitatu na isingejengwa kwa viwango vinavyohitajika.

 “Tumeamua sasa kwenye certificate tunapitia moja baada ya moja kuangalia value for money (mradi kama unaendana na thamani fedha) tumedanganywa vya kutosha hatuwezi kuendelea na kutokana na changamoto hizo tumeamua kuanzisha force akaunti.

“Wizara ya maji ilikuwa haipendwi na hata leo bado kuna watu hawaipendi, wanataka mpemba aondoke,”alisema.

Alisema mara baada ya kuanzisha force akaunti mafanikio yameonekana ambapo miradi kwa sasa inakamilika kwa wakati.

“Tumeanzisha force akaunti na mafanikio tumeyaona, miradi ya force akaunti inatumia miezi mitano hadi sita,    wakati ukimpa mkandarasi anachukua karibuni miaka miwili, mradi unaojengwa kwa force akaunti  kwa Sh bilioni moja mkandarasi atataka Sh bilioni hadi tatu.

“Na mbaya zaidi vifaa anavyoleta yeye ni chini ya kiwango maana kaishatandika huwezi kuona ametandika nini lakini mabomba tunayonunua sisi tunanunua viwandani moja kwa moja matokeo yake tunapata value for money,”alisema.

Udanganyifu katika Miradi

Alisema wakati anaingia katika wizara hiyo  kulikuwa na udanganyifu kati ya wakandarasi na wafanyakazi wenyewe wa wizara.

“Tatizo hilo lilianzia halmashauri, kwenda mkoa hadi wizarani entire system (mfumo wote wa wizara) ya wizara ilikuwa na shida  na hata kama wangelipa bilioni au trilioni kwa system ile wasingeweza kutatua tatizo la maji.

 “Si nia yangu kulaumu mtu yoyote lakini tujifunze kwa makosa yaliyotokea, tukiendelea kusimamia na tukifanya vitu sahihi naamini tutaleta mabadiliko makubwa,”lisema Mbarawa.

Ruwasa Ndio Mwarobaini

Alisema Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (Ruwasa) ndio itakuwa mwarobaini wa kutatua tatizo la maji vijijini.

“Lakini kuna changamoto kwa sababu ni taasisi mpya na tumeleta utaratibu wa kuajiri maofisa manunuzi. Watu wengi wanazungumza lakini miaka mitatu inayokuja tutazungumza mambo tofauti, nimekaa bunge hili miaka 10 bajeti ya maji kulikuwa kuna kelele nyingi lakini leo hakuna,”alisema Waziri Mbarawa.

Changamoto ya miradi kukamilika

Kuhusu baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika, Mbarawa alisema kulikuwa kuna changamoto ya baadhi ya wakandarasi pindi wanapopewa fedha kuzihamisha na kuzipeleka kwenye mambo mengine.

Alisema jambo hilo wizara imelitatua kwa kuwasimamia kwa kuhakikisha fedha zinatumika kwenye miradi iliyokusudiwa.

“Kuna makandarasi  hawapo katika site baada ya kulipwa anaenda kuipeleka hela sehemu nyingine tumewapa muda na tutawafukuza. Na tukiwafukuza tunawapa Ruwasa miradi ya maji sasa imepata mwarobaini,”alisema.

Spika na vijiji kutokupata maji

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema ni kweli kwamba kuna vijiji havijawahi kupata maji na wamekuwa wakitafuta mbinu kuwajibu wananchi hivyo aliiomba Wizara kuwasikiliza na kuwaonea huruma wabunge wanapoomba wapatiwe maji.

“Nakushukuru Profesa umeeleza kwamba system ilikuwa na shida kubwa sana ilikuwa ni cheni ya upigaji wahandisi walikuwa ni sehemu ya wakandarasi.

“Miradi ile ya World Bank (Benki ya Dunia) hakukuwa na wakandarasi wa miradi na  tumepigwa sana hakuna kilichofanyika cheni hiyo ilitengenezwa tangu mwanzo wakandarasi ni wao na wahandisi ni wao na mmejitahidi sana kuuvunja.

“Tunawaunga mkono katika kuelekea katika force akaunti na ndio maana sisi tunapigia mstari mabilioni ya shilingi yamepelekwa lakini thamani ya mradi hakuna. Wizara ya Maji ni shughuli pevu,”alisema Spika.

Aweso na ubambikizwaji wa bili za maji

Awali Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aliwataka wakurugenzi wa mamlaka za maji nchini kusimamia ubambikizwaji  wa bili za maji kwa wananchi  pamoja na kupiga marufuku operation za kukata maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles