22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MBARAKA UKIIHESHIMU MIGUU YAKO ITAKUPA HESHIMA

NA MARTIN MAZUGWA


JIONI ya Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa Tanzania ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burundi mabao yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji, Simon Msuva kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na jingine likiwekwa kimiani na Mbaraka Yusuph, mshambuliaji wa Kagera Sugar.

Ilikuwa ni furaha ya aina yake kwa Watanzania kushuhudia timu yao ya taifa ikitoka kifua mbele dhidi ya Intamba M’urugamba, moja kati ya timu bora kabisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati ambapo katika viwango vya ubora wao wanashika nafasi ya 139 wakati Tanzania inashika nafasi ya 157, mechi ambayo ilikuwa kipimo tosha kwa kikosi cha kocha  Salum Mayanga.

Kwa mara ya kwanza, Mbaraka anaingia katika vitabu vya historia vya soka la Tanzania  kwa kupachika  bao la ushindi  katika mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Taifa,  bao muhimu linaloipa matokeo Taifa Stars katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, nyota huyo wa Kagera Sugar alithibitisha ubora wake na kuwaonyesha Watanzania kuwa hakuitwa kimakosa katika kikosi hicho.

Mshambuliaji huyo ana sifa zote za kuwa mshambuliaji wa mwisho, ni mchezaji aliyekamilika kila idara, ni mtulivu awapo ndani ya boksi pia mwenye uchu pindi anapokuwa katika lango la adui  huku akiwa na jicho kali la kufumania nyavu kwani hadi sasa amepachika mabao kumi katika orodha ya wafungaji VPL akiwa nyuma ya kinara kwa mabao mawili pekee jambo linaloonyesha nyota huyo si wa kubezwa, lakini nyota huyo anajua kukaa katika nafasi pindi timu inapokuwa ikitengeneza shambulizi.

Anachopaswa kufanyiwa Mbaraka ni kuendelezwa zaidi kwa kurekebisha kasoro ndogo ndogo iwapo atafanyiwa hivyo atakuwa hatari zaidi na kuwa na msaada kwa Taifa ambalo hivi sasa limekuwa na tatizo katika safu ya ushambuliaji.

Sina wasiwasi na mahala alipo hivi sasa, yupo katika mikono salama ya mpishi wa vipaji, Mecky Mexime, mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Mtibwa Sugar ambaye hivi sasa ni moja ya makocha bora zaidi katika ardhi ya Tanzania ambaye ameibua nyota wengi wanaotamba Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mbaraka unapaswa kuiheshimu miguu yako iliyokupa heshima na kuliweka jina lako kwenye ramani ya soka mfano mzuri ni nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa, Mbwana Samatta, ambaye ameamua kuiheshimu miguu yake ambayo hivi sasa imempa heshima hapa nchini barani Afrika pamoja na ulimwenguni kote lakini pia imemfanya kuwa lulu barani Ulaya ambako amekuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Genk ambao kila kukicha wanaliimba jina lake.

Unapaswa kutunza miguu yako kama mboni ya jicho lako ambayo hata ikipitiwa na upepo huifumba kuikwepesha isipate tatizo  kama utayafanya haya na kuongeza juhudi zaidi naamini tutakuwa tumetibu tatizo sugu la nafasi ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikilitesa soka la Tanzania.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles