OSLO, Norway
KIONGOZI wa upinzani Venezuela, Juan Guaido amesema mazungumzo yanayoandaliwa na Norway baina ya wajumbe wake na wa Rais Nicolas Maduro yataendelea, licha ya awamu ya kwanza kumalizika bila maafikiano yoyote jana.
Guaido ameishukuru Norway kwa juhudi zake za kuchangia katika kuutafutia suluhu mzozo wa Venezuela, akiongeza kuwa yuko tayari kuendelea kutoa ushirikiano.
Rais Maduro pia ameunga mkono njia hiyo ya mazungumzo katika hotuba yake iliyotangazwa kupitia televisheni.
Katika hotuba hiyo, rais huyo alisema ana imani katika mjadala, katika kuheshimu katiba na katika amani na demokrasia.
Wawakilishi wa pande hizo mbili katika mzozo wa siasa Venezuela wamekuwa wakikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza mjini Oslo.
Hata hivyo mazungumzo yao yalimalizika bila makubaliano yoyote.