23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MAYWEATHER AVURUGA NDOA YA T.I NA TINY HARRIS

ti

Na BADI MCHOMOLO

MWAKA 2016 unamalizika leo hii, kuna watu ambao wanafurahia leo hii kumaliza mwaka salama huku wakiwa wametimiza malengo yao, lakini wapo ambao wanamaliza mwaka huu huku wakiwa katika wakati mgumu.

Rapa Clifford Harris maarufu kwa jina la T.I ni miongoni mwa wasanii ambao wanamaliza mwaka huku wakiwa katika wakati mgumu, hii inatokana na mke wake Tameka Cottle, kuweka wazi kuwa anataka talaka kutoka kwa baba wa watoto wake watatu.

T.I alifunga ndoa na mrembo huyo ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Marekani tangu mwaka 2010, lakini walikuwa katika uhusiano kuanzia mwaka 2001 na kufanikiwa kupata watoto watatu – wawili wa kiume na mmoja wa kike.

Chanzo cha mgogoro wa wawili hao kinadaiwa kuwa ni bilionea Floyd Mayweather, bingwa wa mchezo wa ngumi, ambaye hana maelewano mazuri na rapa huyo kwa kipindi kirefu sasa.

Mwezi Novemba, mwaka huu mke wa T.I alikuwa jijini Las Vegas ambapo alipata mwaliko kwenye ‘Bush’ ya nyota wa muziki nchini Marekani Mariah Carey.

Katika sherehe hiyo ya Mariah, ilionekana kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo nyota wa ngumi duniani Mayweather.

Katika kupiga picha za Selfie, mke wa T.I alionekana akipiga picha na bondia huyo ambapo picha hiyo ilisambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kitendo hicho kilimfanya rapa T.I ajisikie vibaya na kukosa kabisa amani kwa kuwa nyota huyo wa muziki wa Hip Hop ana bifu kubwa na bondia hiyo, ambapo T.I aliwahi kuweka wazi kuwa yupo tayari kupigana na bondia huyo popote watakapokutana.

Hilo ni bifu ambalo limedumu kwa muda mrefu, hivyo kitendo cha mke wa T.I kupiga picha na Mayweather kimeleta msuguano kila siku ndani ya nyumba ya wasanii hao, hivyo inadaiwa kwamba Tameka amechoshwa na maneno ya kila siku kutoka kwa rapa huyo hivyo ameona bora adai talaka.

Kutokana na hali hiyo ni wazi kwamba T.I ataendelea kujenga uhusiano mbaya na bingwa huyo wa ngumi duniani, kikubwa ni kwamba kwenye mitandao ya kijamii inamwangalia msanii huyo analichukuliaje suala hilo?

Kwa upande wa Mayweather, amekuwa bondia ambaye anapenda sana wanawake warembo, amekuwa akihusishwa kutoka na warembo mbalimbali hasa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Inadiwa kwamba endapo anampenda mrembo yeyote yupo tayari atumie kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kutoka naye hata kama yupo mbali na nchini Marekani ambapo Mayweather anaishi, yupo tayari kutuma ndege maalumu kwa ajili ya kumfuata mrembo ambaye anataka kutokana naye na baadaye anapiga picha ambazo zinaonesha wazi kuwa alitoka naye.

Mayweather baada ya kutangaza kustaafu ngumi, aliweka wazi kwamba kilichobaki kwake ni kufanya starehe, hivyo aina yenyewe ya starehe ni pamoja na kutoka na warembo mbalimbali.

Kutokana na kauli hiyo, leo hii ukiona bondia huyo amepiga picha na mpenzi wako ni kitu cha kujiuliza mara mbilimbili japokuwa inawezekana ikawa ni picha ya kawaida tu isiyo na madhara yoyote.

Hadi sasa T.I hajataka kuweka wazi juu ya kuenea kwa taarifa hizo, lakini kwa upande wa watu wa karibu na familia hiyo, wamedai kuwa mke wa T.I yupo tayari kuondoka na anataka talaka, yote hayo ni kutokana na Mayweather.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles