30.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Mayweather amchapa Nasukawa kwa KO

TOKYO, JAPAN

BINGWA wa ngumi duniani, Floyd Mayweather, juzi alitumia sekunde 140 kumaliza pambano dhidi ya mpinzani wake, Tenshin Nasukawa na kufanikiwa kuondoka na kitita cha dola milioni 9, zaidi ya bilioni 20.

Pambano hilo lilifanyika jijini Tokyo, huku Nasukawa akitamba kufanya makubwa mbele ya mashabiki wake, lakini alipokea kichapo raundi ya pili na kumaliza pambano hilo.

Mayweather mwenye umri wa miaka 41, alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo huku akiamini kuwa ana uwezo wa kulimaliza mapema na hatimaye alimwangusha chini mara tatu mpinzani wake huyo mwenye umri wa miaka 20.

Pambano hilo lilimalizika baada ya kikundi cha Nasukawa kudondosha kitambaa cheupe ulingoni wakimaanisha kusitisha pigano hilo kutokana na ngumi mzito alizokuwa anapigwa kijana huyo, hata hivyo, Nasukawa alionekana akibubujikwa na machozi.

Mayweather tayari alistaafu ngumi tangu Agosti 2017 baada ya kumchapa mpinzani wake bingwa wa UFC, Conor McGregor, lakini juzi aliamua kurudi ulingoni akidai kuwa ni sehemu ya kuwapa burudani mashabiki wake, lakini yeye amestaafu ngumi za kulipwa.

”Ni sehemu ya kuburudisha tu mashabiki, nimefanya hivi kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wangu wa hapa nchini Japan, walikuwa wanataka kuona yakitokea haya nikasema kwanini nisifanye hivyo, lakini mpinzani wangu bado ni bingwa wa ngumi.

“Nataka niwahakikishie kwamba mimi nimestaafu ngumi za kulipwa, lakini nataka kutumia nafasi hii kuwaambia mashabiki wa Nasukawa kuendelea kumsapoti ana uwezo mkubwa ninaamini atakuja kuweka historia,” alisema Mayweather.

Nasukawa anajulikana kuwa ni bondia wa Kickboxer ambaye amekuwa akitumia na mateke, lakini katika pambano hilo alipewa masharti magumu kwamba akionekana anarusha teke basi atatozwa faini ya dola milioni 5, ambazo ni zaidi ya bilioni 11.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba, Mayweather alionekana kuwa na uzani wa juu kwa kilo nne dhidi ya mpinzani wake, hivyo wataalamu wa ngumi walilikosoa pambano hilo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,464FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles