Mayanja: Siku hazifanani

0
516

IMG_6415

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ametetea matokeo ya sare ya bao 1-1 ambayo timu yake ilipata juzi dhidi ya URA ya Uganda kwenye pambano la kirafiki la kujiandaa na msimu mpya kwa kusema kuwa siku hazifanani.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja alisema Waganda hao walikuwa kipimo tosha kwa timu yake kutokana na upinzani mkubwa waliowapa.

“Mchezo ulikuwa mzuri kwa pande zote mbili kwani wachezaji wote walipambana katika kuhakikisha wanapata ushindi, lakini mwisho wa siku tukatoka sare ya bao 1-1,” alisema Mayanja.

Mayanja aliendelea kusema kuwa kupitia pambano hilo kocha mkuu, Joseph Omog, ameshafahamu kikosi chake cha kwanza ambacho atakuwa akikitumia kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Sare ya URA imekuja siku chache baada ya miamba hiyo ya Msimbazi kuichapa AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 4-0 katika pambano la kujipima nguvu lililochezwa siku ya tamasha la Simba.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa URA, Kefia Kisala, alisema Simba ya sasa ipo tofauti sana na ya miaka ya nyuma.

“Mchezo ulikuwa ni mzuri, kila timu ilipambana lakini kutokana na kuwafahamu vizuri Simba, tulibadilisha mfumo tuliocheza na Azam FC ili kuwakabili na kufanikiwa kutoka sare ya bao 1-1,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here