25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mayanja aeleza atakavyoimaliza AS Kigali Dar

MOHAMED KASSARA – DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja amesema kwa sasa anafanya kazi ya kukiongezea kasi kikosi chake, kwa ajili ya kuhakikisha kinawapeleka mchaka mchaka wapinzani wao AS Kigali, katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.

KMC ilizindua vema kampeni zake ugenini kwa kulazimisha suluhu dhidi ya AS Kigali ya Rwanda, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali uliochezwa wiki iliyopita Uwanja wa Nyamirambo nchini humo.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema licha ya wachezaji wake kucheza vizuri mchezo wa kwanza, lakini amebaini hawana kasi ya kutosha inayoweza kumsababishia mpinzani kufanya makosa.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu kuelekea mchezo huo, vijana wote wako salama, wanajituma mazoezini, tunatarajia kila kitu kitakwenda sawa, tunajifua kulingana namna tulivyowaoana wapinzani wetu wakicheza.

“Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza, lakini mchezo wa marudiano kuna vitu tunapaswa kuviongeza, nimegundua tutakiwa kuboresha kasi yetu ili kutompa mpinzani mwanya wa kupumzika, hiyo itatusadia kumfanya achoke na kufanya makosa mengi, pia tunatakiwa kuongeza umakini kwenye ushambuliaji ili kutumia vema nafasi zote tutakazopata kufunga mabao,”alisema kocha huyo raia wa Uganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles