26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mawaziri wakutana kuimarisha mikakati ya kudhibiti ukatili kwa watoto

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amehimiza ushirikishwaji wa wadau wote katika kuunganisha nguvu ili kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiongoza kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa kisekta kilichofanyika leo Desemba 21, jijini Dar es Salaam, kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Doroth Gwajima (kulia) katika kikao hicho.

Waziri Simbachawene, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na wataalamu waandae miongozo yote izungumze kwa pamoja kuhusu ukatili wa kijinsia na baada ya kikao cha Mawaziri ushauri upelekwe kwa Waziri Mkuu ili aridhie.

Ili hatua za muda mfupi hatua za muda wa kati na hatua za muda mrefu ziweze kuchukuliwa katika kupambana na vita hii, binadamu wamekuwa waajabu kuliko wanyama matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanywa na ndugu wa karibu.

Katika kikao hicho amesema Mwaka 2021 viliripotiwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto 110,499 ikiwa ni asilimia chache yawalioripoti.

“Ulioongoza ni ukatili wa ubakaji 5,899 na waliolawitiwa 1,114 na waliopata mimba za utotoni ni 1,677 na utafiti ukaonesha namba hizi uzigawe kwa 60, utaona asilimia 60 inafanyika nyumbani walipo baba na mama, ndugu jamaa na marafiki na asilimia 40 ni nje ya nyumbani, wakiwa shuleni au wanapoenda shuleni,” amesema Simbachawene.

Upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dk. Dorothy Gwajima amesema lazima kuimarisha mifumo izungumze na uwajibikaji, sheria tunazo tayari tunamiongozo mbalimbali sasa tunahitaji mawasiliano yaanzie kwa Mawaziri yashuke kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, ishuke kwenye kata zetu, ishuke kwenye mitaa na vijiji.

“Mfumo wa mawasiliano uende kwenye kamati za mabaraza ya madiwani kwenye Halmashauri zetu, lakini kwenye vikao vya maendeleo vya kata ili viwe na nguvu ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ili hata marekebisho ya sheria ndogo ndogo yaanzie kule chini,” amesema Waziri Gwajima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles