24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mawaziri, wabunge vinara wa kuhudhuria vikao vya bunge watajwa

Fredy Azzah, Dodoma



Baada ya kutaja mawaziri na wabunge watoro wa vikao vya bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja majina mengine ya wabunge na mawaziri ambao wamekuwa na mahudhurio mazuri kwenye vikao vya kamati za bunge na vikao vya Bunge.

Ndugai amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Novemba 15, na kuongeza kuwa orodha hiyo inatokana na maudhurio ya wabunge na mawaziri kwenye mkutano wa 11 ambao ulikuwa wa Bunge la Bajeti ule wa 12.

Spika Ndugai ametaja mawaziri wenye mahudhurio mazuri zaidi kuwa wa kwanza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. AShatu Kijaji, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusuph Masauni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.

Kwa upande wa wabunge wenye mahudhurio mazuri kwenye kamati za bunge na vikao vya bunge, wa kwanza ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Justine Monko (CCM), Felister Bura, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mbunge wa Kilindi, Omary Kigua (CCM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles