24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

MAWAZIRI SABA WAKUTANA KUDHIBITI WAVUVI HARAMU

0-1uvuvi-haramu-mkoani-mwanza-6

Na ASHA BANI – Dar es Salaam

MAWAZIRI saba na wataalamu mbalimbali walikutana jana Dar es Salaam kujadili mikakati na mbinu za kudhibiti uvuvi haramu.

Wizara zilizoshiriki ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Nishati na Madini.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Waziri Makamba, alisema lengo la kukutana ni kuweka mikakati ya kudhibiti wavuvi haramu wanaotumia milipuko ya mabomu.

Makamba alisema kwa miaka kadhaa sasa uvuvi haramu  umeshika kasi na kufanya ongezeko la uharibifu wa masalia ya viumbe hai baharini.

Alisema wamekaa na kujadili mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hatua za tahadhari kwa kila wizara mtambuka kufanya kazi yake ya ulinzi huo.

“Hiki ni kikao cha kazi zaidi na mikakati yake mbalimbali sambamba na mbinu za kuwakabili wavuvi haramu na ni lazima kwa Serikali makini itafanikiwa katika hili,’’ alisema Makamba.

Makamba alisema baada ya miezi sita, watatoa hatima ya vikao na majibu ya nini kitafanyika katika kupambana na uvuvi huo haramu ambao umeundiwa timu maalumu.

 TIZEBA

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Tizeba, alisema uvuvi haramu una athari kubwa kwa mazalia ya uvuvi na si samaki tu bali hata uharibifu wa mazingira.

Alisema asilimia 40 ya eneo la bahari limeharibiwa na wavuvi haramu na kama hakutakuwa na uthubutu wa kuzuia, basi ifikapo mwaka 2020-2025 hakutakuwa na mazalia yoyote.

Dk. Tizeba alisema endapo uvuvi wa kutumia mabomu na baruti na mbinu nyingine haramu utaongezeka katika eneo ambalo limeathiriwa, uwezekano wa kurudi upya ni katika kipindi cha miaka 70 hadi 100 ijayo jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

“Na kama Serikali haitafanya jitihada ya makusudi kudhibiti hali hiyo, basi kutakuwa na athari kubwa kiuchumi na kijamii pia watu kudumaa kwa kula vyakula vyenye sumu,” alisema.

 MWIGULU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu, alitoa rai kwa Watanzania kila mmoja awe na wajibu wa kulinda rasilimali hizo.

Alisema ubaya wa kuachwa huru watu hao kuna madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kufanya uharibifu wa mazalia sambamba na samaki wadogo.

 JAFO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jafo, alisema kama suala hilo linaendelea kwa kasi kuna haja ya kuwatumbua wakurugenzi na maofisa uvuvi.

“Maofisa uvuvi ni lazima kuwatoa kwenye nafasi zao kwa kuwa wanaohusika ni wao kwa usimamizi licha ya watendaji wengine kuanzia ngazi za chini kuhusika na suala la kuhujumu,’’ alisema Jafo.

Aliwataka wenyeviti wa Serikali za mitaa wanapokuwa kwenye vikao vyao mbalimbali vya utendaji, ajenda yao ya kwanza iwe ni kudhibiti uvuvi haramu.

 PROFESA MAGHEMBE

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Maghembe, alisema kuna hifadhi za taifa hapa nchini ambazo zipo katika nafasi ya 300 ya ubora duniani lakini kutokana na uvuvi haramu ni lazima kutaharibika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles