32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mawaziri, manaibu kuwa 40

Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge
Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge

NA DEBORA SANJA, DODOMA

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge amesema Katiba inayopendekezwa imeongezwa masuala kadhaa ikiwamo ukomo wa mawaziri na manaibu wao ambao sasa hawatazidi 40.

Mbali na hilo, alisema idadi ya wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa watakuwa 340 hadi 390.

Chenge aliyasema hayo jana mjini hapa ambapo aliweka wazi kuwa mabadiliko hayo yametokana na Rasimu ya Katiba ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Katiba inayopendekezwa imezifanyia marekebisho ibara 200 zilizokuwa katika rasimu, imefuta ibara 29, imeongeza ibara mpya 54 na haijafanya marekebisho yoyote kwa ibara 42 za rasimu,” alisema.

Chenge alisema Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa na sura 17 na ibara 271, lakini Katiba inayopendekezwa ina jumla ya ibara 296 na sura 19.

“Bunge Maalumu la Katiba lilifanya maboresho ya msingi ambayo ni pamoja na kubadili muundo wa Muungano uliopendekezwa na tume wa Serikali tatu na kuweka Serikali mbili.

“Kutokana na maboresho hayo, baadhi ya ibara ziliathiriwa ili kukidhi mahitaji ya Serikali mbili,” alisema Chenge.

Alisema Bunge Maalumu la Katiba limeweka nyongeza ya mambo matatu ambapo ya kwanza inaweka utaratibu wa kubadilisha masharti ya Katiba kuhusu mambo ya Muungano.

“Nyongeza nyingine inahusu mambo machache ambayo mabadiliko yake yatahitaji maoni ya wananchi kupitia kura ya maoni na nyongeza nyingine imeainisha mambo 16 ya Muungano,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles