30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAZIRI, AG Z’BAR WAMVAA PROF. KABUDI


Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

SIKU chache baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, kulieleza Bunge kwamba Rais Dk. John Magufuli ana mamlaka yote ya kutoa maagizo kwa mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), suala hilo sasa limetua ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Wakati Baraza hilo likiendelea na vikao vyake jana mjini Unguja, mawaziri wa SMZ walimvaa waziri huyo, baada ya Mwakilishi wa Chaani, Nadir Abdul-Latif Yussuf (CCM), kuwasilisha hoja ya dharura kuhusu kauli ya Profesa Kabudi na kudai kuwa inakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Kutokana na hoja hiyo, upande wa Serikali walilazimika kutoa ufafanuzi.

Aliyekuwa wa kwanza kujibu hoja hiyo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa SMZ (AG), Said Hassan Said, ambaye alisema nchi huongozwa kwa kuzingatia masharti ya Katiba na sheria ambazo zinatungwa na Baraza la Wawakilishi au Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzingatia masharti ya Ibara 64 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo imetoa mamlaka kwa Bunge kutunga sheria ambazo ni za Muungano.

“Lakini pia kutunga sheria ambazo si za Muungano, ambazo zinatekelezwa Tanzania Bara. Pia tujue Mheshimiwa Naibu Spika kama nguvu za kutunga sheria kwa mambo ambayo si ya Muungano yako mikononi mwa Baraza la Wawakilishi, kwa mujibu wa kifungu cha 77 cha Katiba ya Zanzibar.

“Sasa tuondowe hofu waheshimiwa wajumbe, mambo haya yanapozungumzwa majibu yake ni kama haya ambayo waheshimiwa wajumbe wameyajibu. Mtu anapozungumza wewe mwelekeze kwenye masharti ya sheria na masharti ya Katiba ndiyo nchi inavyoongozwa. Nchi haiongozwi kwa maagizo kwa sababu utekelezaji wake ni wa kisheria,” alisema Mwanasheria Said.

Hata hivyo, alisema kama agizo limetoka, utekelezaji wake unahitaji kutekelezwa kwa sheria ambayo imetungwa na Bunge, litatekelezwa na kama limetoka kwa maagizo yaliyotokana na sheria ambazo utekelezaji wake unahitaji matekelezo ya Baraza la Wawakilishi, zitatekelezwa.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles