25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mawasiliano hafifu chanzo cha migogoro’

Na AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MENEJA wa Idara ya Ustawi wa Ajira kutoka Kampuni ya AAR, John Ngonyani amesema kuwa wanandoa wanaongoza kukumbwa na msongo wa mawazo ambao unasababishwa na migogoro huku chanzo kikiwa ni  mawasiliano haba baina yao.

Ngonyani ambaye pia ni mwanasaikolojia, amesema utafiti uliofanywa na AAR tangu mwaka 2012 iliponzishwa,  miongoni mwa kesi zinazoongoza kusababisha msongo wa mawazo hadi sasa ni ndoa na mahusiano ya kimapenzi.

Akizungumza na MTANZANIA jana Dar es Salaam katika mahojiano maalumu, alisema urafiki kati ya wanandoa ni namna bora ya kudumisha mahusiano mazuri baina yao.

“Ndoa nyingi zinakuwa na changamoto sababu kubwa ni  mawasiliano, kingine hakuna urafiki kati ya wanandoa, hili ni tatizo kwani moja ya kitu kinachofanya mahusiano bora katika ndoa ni urafiki, msipokuwa marafiki uhusiano unakuwa na changamoto kubwa.

“Wanandoa wanatakiwa kuwa na ukaribu unaoweza kuzalisha hisia, hii ni sehemu ya kuongeza upendo (Triangle of love), hapa nikimaanisha urafiki, hisia na uelewano baina yao kwani kufa kwa urafiki kati ya wanandoa kunaenda kuua hisia,” alisema Ngonyani.

Alisema sababu zingine za migogoro ya ndoa ni kukosa uaminifu baina ya wanandoa, hivyo hali hiyo kusababisha msongo wa mawazo kati yao.

“Kutomwamini mwenzako katika ndoa kunaweza kukufanya ukawa na msongo wa mawazo, na pia tabia za udanganyifu zinaweza kuwa tatizo kwa wanadoa, inatakiwa  watu wakae pamoja kwa sababu ya upendo, lakini wengine wanaishi tu ili kulea watoto,” alisema Ngonyani.

Alieleza kuwa mtu anaweza kuepuka msongo wa mawazo kulingnaa na jinsi atakavyopokea jambo ambalo linamsababishia msongo wa mawazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles