25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakili watano kutetea ubunge wa Kubenea

said1NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MWANASHERIA Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa kuongoza jopo la mawakili watano watakaomtetea Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) katika kesi ya kupinga ubunge wake.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Massaburi.

Kubenea aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na MTANZANIA baada ya Massaburi kufungua shauri la madai namba 8 la mwaka huu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Washtakiwa  katika kesi hiyo ni Kubenea, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ubungo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mbunge huyo wa Ubungo alisema   kwa kuwatumia wanasheria wake wamejibu hoja 11  ambazo zitawasilishwa mahakamani wiki hii.

“Jopo la mawakili wangu wamefanyakazi ya kujibu na naamini kesi hiyo itaisha katika hatua za mwanzo  maana nina imani kubwa na kazi ya wanasheria wangu ambao ni Tundu Lissu, Mabere Marando, Peter Kibatala, Method Kimomogolo na Fredrick Kihwelo,” alisema.

Kubenea alisema katika madai waliyomtumia ameona hakuna madai ya msingi miongoni mwa madai hayo 11 yaliyotolewa na mlalamikaji.

Alisema miongoni mwa madai hayo, Massaburi ambayo anapinga ubunge wake ni kwamba waliruhusiwa wapiga kura ambao walikuwa hawakidhi umri halali wa kupiga kura ambao mwenyewe mlalamikaji aliwashuhudia.

Dk. Massaburi anadai kwamba msimamizi hakumuarifu kuhusu muda, mahali au tarehe ya sehemu yalikokuwa yakifanyika majumuisho ya mwisho ya kura za uchaguzi huo mkuu.

Vilevile Dk. Massaburi anadai kuwa yeye na mawakala wake hawakuruhusiwa kuona vifaa vya kupigia kura kama ilivyofanyika kwa Kubenea na mawakala wake.

Pia anamlalamikia Kubenea kwa  kutoa rushwa ya   jenereta katika hospitali ya Mavurunza eneo la Kimara, zawadi ya meza ya mchezo wa pool  kwa vijana wa Makuburi na kujenga barabara ya Matete eneo la Kimara akiwashawishi kumchagua.

Katika madai hayo amemlalamikia msimamizi kukataa kuhakiki kwa mara ya pili matokeo yake ikiwamo na watu kadhaa wa maeneo ya Mizizini, Mianzini, Kilimahewa, Mizambarauni, Shule ya Mugabe na Kanuni, kutopiga kura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles