25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakala wahimizwa kutumia mbegu zilizosajiliwa

FLORANCE SANAWA, MTWARA

Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu nchini kanda ya kusini (TOSC), imehimiza mawakala kusambaza mbegu zilizothitishwa na taasisi hiyo.

Akizungumza na mawakala hao Mkaguzi wa TOSC, Neema Yohana amesema kwakushirikiana na vyama vya mawakala kwa mikoa ya lindi na mtwara wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa mawakala wa mbegu kwa mikoa hiyo.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwaelimisha kutambua mbegu bora na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbegu hizo ili kuleta tija kwenye kilimo nchini.

”Sisi tunalenga kuwaelimisha ili kujua mbegu bora ambayo kwa sasa iko kama vocha ya kukwangua mbegu na tunatamani kila mkulima apate mbegu hizo zilizosajiliwa.

“Mara nyingi tunafanya majaribio ya watalaam na tunapokea kutoka kwa watafiti mbalimbali, zikaguliwe na zifikishwe kwa mawakala kwa wakati ili waweze kuzisambaza kwa wakulima” amesema.

kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mawakala wa Pembejeo za Kilimo (LIADA), Said Kinyonga amesema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakiathirika kwa matumizi ya mbegu zisizo na tija ambazo hazijathibitishwa na TOSC.

“Mafunzo haya ni muhimu kwetu na yanatujenga kitendo cha sisi na kutupa ufahamu ambao unatujenga na kutufanya tutambue mbegu zipi bora zipi sio bora hii itawafanya wakulima wengi kuacha kulima kwa mazoea kwa kutunza mbegu ambazo ndio tulivyokuwa tukifanya zamani” amesema Kinyonga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles