27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mawakala Al-Shabaab wapewa hati ya mashitaka

Kundi la Al-shabaab
Kundi la Al-shabaab

NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imewapa hati ya mashitaka watuhumiwa 16 wanaodaiwa kuwa mawakala wa kundi la Al-Shabaab kwa kusajili vijana kujiunga na kundi hilo na mauaji na kujaribu kuua katika mlipuko wa bomu uliotokea Baa ya Arusha Night Park, jijini Arusha.

Watuhumiwa hao walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Msofe na kesi yao ilikuwa inatajwa huku wote wakionekana wamevalia vazi la kanzu.

Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri, Gaudencia Joseph, mbele ya Hakimu Mkazi Msofe, alidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo aliiomba Mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo wakati Mwendesha Mashitaka akimalizia kutoa maelezo yake, mmoja wa watuhumiwa alinyoosha mkono kwa ajili ya kuomba kuuliza swali ambapo ilikuwa hivi;

Mtuhumiwa: Hati ya Mashitaka

Hakimu: Imefanya nini?

Mtuhumiwa: Tunaomba kupatiwa Hati ya Mashitaka (Charge Sheet)

Hakimu: Upande wa Mashitaka mna jambo la kuzungumza?

Mashitaka: Sina Mheshimiwa.

Hakimu: Kwa vile kuna nakala ya hati hapa, Mahakama itawapatia nakala moja ya hati ya mashitaka.

Mtuhumiwa: Kesi hii haina dhamana?

Hakimu: Haina.

Kutokana na ombi la kupatiwa Hati ya Mashitaka, Hakimu Mkazi Msofe aliwapatia watuhumiwa hao nakala moja kama walivyokuwa wameomba. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.

Watuhumiwa hao walipofikishwa mahakamani wiki mbili zilizopita walilalamika mbele ya Hakimu Msofe, wakidai tangu walipokamatwa hawajawahi kupewa hati ya mashitaka.

Katika hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, ilikuwa dhidi ya watuhumiwa 16 wanaokabiliwa na tuhuma za kujibu mashitaka 16 ya kuua, kujaribu kuua na kushawishi vijana kujiunga na kusaidia kikundi cha kigaidi cha Al- Shabaab.

Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Khalili Muda, aliwasomea mashtaka ya kuua watuhumiwa tisa kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua Sudi Ramadhan, aliyekuwa majeruhi wa bomu lililotokea Baa ya Arusha Night Park kisha kuendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Mkoa wa Arusha ambaye baadaye alipoteza maisha Mei 13, mwaka huu.

Mwendesha Mashitaka Muda aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Abdallah Athumani Labia (34) mkulima na mkazi wa Mang’ola wilayani Karatu, Abdulkarim Thabit Hasia (32) Mkazi wa Ngusero, Hassan Zuberi Saidi (28) mkazi wa Tengeru na Rajab Phiri Hemedi (28) mkazi wa Magugu Babati.

Wengine ni Ally Hamisi Kidaanya (32), mkazi wa Magugu-Babati, Abdallah Maginga Wambura (40), mkazi wa Kwa Mromboo-Murriet, Shabani Abdallah Wawa (22), mkazi wa Magugu-Babati, Ally Hamisi Jumanne (25), mkazi wa Matufa-Babati na Yassin Hashim Sanga (26), mkazi wa Kahama.

Watuhumiwa wengine ni Abdallah Maginga Wambura aliyesomewa mashtaka yake akiwa Hospitali ya Mount Meru wakati mtuhumiwa Abdulkarim Thabit Hasia hakusomewa mashtaka yake kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Mwendesha Mashitaka katika hati hiyo aliendelea kudai kwamba kati ya mwaka 2010 hadi Februari mwaka huu maeneo mbalimbali nchini, watuhumwa Swalehe Hamisi (51) mkazi wa Sombetini, Abdallah Yassin (33), mkazi wa Tunduru na Sudi Nasibu Lusuma (18), mkazi wa Mwanza waliwashawishi watu wajiunge na kusaidia kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Alidai kitendo hicho ni kinyume na kifungu 118 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002 ambapo watuhumiwa hao walijaribu kusajili watu kujiunga na kikundi hicho kinyume cha kifungu namba 21 (a) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. Mimi sioni haja ya kufanya makesi na mtuhumiwa yeyote wa ugaidi na kuanza kuhangaika kutafuta ushahidi.Ni vema yeyote anayeshukiwa kuwa ni gaidi akikamatwa atwangwe risasi mara moja bila kwenda kubishana naye mahakamani maana watashinda tu.Ni vizuri serikali kama kweli ina nia ya dhati ya kukomesha vitendo vya ugaidi nchini ichukue maamuzi magumu kama hayo.

    • Matokeo yanaonyesha kuwa kila hatu ya kupambana na magaidi inapokithiri ndipo wanapozaliwa wengi zaidi. na hatua ya kuwakamata inawapa mwanya wa kutafuta njia bora ya kutekeleza matakwa yao. Sioni kama serekali inachukua hatua stahili kwani Kenya nao walifanya hivyo hivyo lakini matokeo yake yalikuwa mabaya zaidi na maelfu ya rai wa kenya wanaishi kwa wasiwasi huku viongozi wa kisiasa wakiwa na ulinzi wa kutosha.

  2. Magaid mnawajua nyie?Bush obama netanyahu ….na waliopeleka majeshi yao nch za KIISLAM.Yani nyinyi muue wenzenu2 nao wakijitetea mnawanyamazisha kwa kuwaita magaid kumbe nyinyi ndio haswa….

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles