24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mavunde: majimbo ya Ubungo, Kibamba 2020 lazima yarudi CCM

Na Asha Bani-Dar Es Salaam

Naibu  Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amesema mwaka 2020 ni lazima majimbo mawili Ubungo na Kibamba yarudi  ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza leo Mei 26, kwenye kampeni maalum inayoendeshwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema CCM itahakikisha Dar es salaam inakuwa ya kijani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

“Kama kuna uhitaji wa maji, barabara nzuri vyote vinafanyika sasa kuna haja gani ya kubakia upande wa pili wa upinzani ni lazima vijana kufanya kazi kuhakikisha majimbo yanarudi CCM na katika uchaguzi wa serikali za mitaa kata zote ziwe chini ya chama chetu.

“Jitahidini viongozi hii ni aibu anzeni na mitaa yote 91 kuhakikisha inarudi ndani ya CCM maaana nikiangalia hapa hakuna kupita Mnyika wala Kubenea watapitia wapi?,’’amesema Mavunde.

Aidha Waziri huyo amesema makosa yalifanyika hapo awali yakuachia majimbo hayo kuchukuliwa na chama cha upinzani chini ya Mbunge, John Mnyika (Kibamba ) na Mbunge, Saed Kubenea (Ubungo), hayatafanyika tena kwa kuwa hakuna wanachokifanya zaidi ya kutekeleza ilani ya CCM.

Katika hatua nyingine Mavunde aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kujiajiri wakati wakisubiri mchakato wa serikali katika kuongeza ajira kwa vijana hao.

“Vijana wa Ubungo na Kibamba wakati mkiwa mnasubiri mchakato wa serikali wa kuongeza ajira kwa vijana, ni wakati wenu wa kuunda vikundi  vya ujasiriamali vya kukopeshana ili muweze kupata fedha kwani maeneo haya yana fedha nyingi ambazo zimetengwa kwa ajili yenu,” amesema Mavunde- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,222FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles