29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mavunde azindua rasmi Program ya ‘Kijanisha Maisha’

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo (PASS Trust) imezindua rasmi program ya ‘Kijanisha Maisha’ kwa lengo la kuongeza uungaji mkono wa ajenda ya ukuaji wa kijani shirikishi kwa kilimo endelevu nchini Tanzania.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo Februari 24, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde.

Akizungumza katika mkutano huo Mavunde ambaye alimuwakilisha Waziriwa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa uzinduzi wa programu ya kijanisha maisha iliyozinduliwa na Taasisi ya Pass Trust alitoa pongezi juu ya kuja na mpango wa kukuza uchumi kupitia ajenda ya ukuaji wa kijani shirikishi, amesema ni njia bora ya kuchochea kilimo endelevu.

“Naipongeza PASS Trust kwa ubunifu na kuanzisha ajenda ya ukuaji wa kijani shirikishi ambayo kwa hakika inachochea maendeleo endelevu ya kiuchumi ambayo yanaenda sambamba na utunzaji wa mazingira na kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo,” amesema Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde ameipongeza taasisi hiyo kwa malengo mazuri ya kumuunga mkono Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuboresha sekta ya kilimo nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Ibrahim Kaduma amesema: PASS Trust inamchango mkubwa katika kuchochea na kuwezesha ukuaji wa kilimo nchini Tanzania huku tukitoa kipaumbele kwa vijana na wanawake ambapo tunawapa dhamana ya mikopo na huduma za maendeleo ya biashara ili kufikia malengo yao,” amesema Ibrahim.

Ameongeza kuwa PASS Trust ilianzisha kampuni tanzu ya PASS Leasing ambayo inatoa zana zote za kilimo kutoka kwa wauzaji mbalimbali washirika nchini Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles