29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MAVUNDE ATOA AHADI KUNUNUA GARI LA MAITI

Na TAUSI SALUM -DODOMA


MBUNGE wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde (CCM), ameahidi baada ya mwezi mmoja kununua gari la kubeba maiti katika mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Kauli hiyo aliitoa jijini hapa juzi wakati akizindua kambi ya upimaji macho, upasuaji na utoaji wa miwani bure katika hospitali hiyo ikiwa ni mpango wa kuendelea kuwasaidia wananchi wenye matatizo kiafya.

Alisema gari hilo litatumika na mwananchi yeyote aliye mkoani hapa kupeleka maiti katika eneo lolote ikiwa atatoa gharama ya fedha kwa dereva na mafuta.

“Pamoja na shughuli hii, niseme tu baada ya mwezi mmoja ofisi yangu italeta gari kwa ajili ya mwananchi yeyote hapa jimboni kwangu atakayehitaji kusafirisha msiba kwenda sehemu yoyote hapa Dodoma, atachangia gharama ya mafuta na dereva tu,” alisema.

Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, alisema tatizo la macho kwa Dodoma limekuwa kubwa kutokana na mazingira halisi ya mkoa huo.

Aliwataka wananchi mkoani hapa kuwa na tabia ya kuchunguza afya ya macho mara kwa mara ili kuwa salama.

“Mazingira tunayoishi yanasababisha magonjwa ya macho na sisi watu wa Dodoma tunaongoza kwa magonjwa ya macho kutokana na uhalisia wa mazingira na hali ya hewa ya mkoa wetu, hivyo tunapaswa kuwa makini na hili,” alisema.

Kwa upande wake, Mratibu wa shughuli hiyo, Dennis Nachipyangu, alisema hadi sasa watu 600 wamejitokeza kupima na kupatiwa matibabu ya macho bure.

Baada ya vipimo, alisema watu 20 wanatarajiwa kuingia katika chumba cha upasuaji wa macho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles